2013-03-13 19:31:54

KANISA LIMEPATA PAPA MPYA


Ilikuwa ni saa 1:06 wakati moshi mweupe ulipotoka kwenye paa la Kikanisa cha Sistina, ishara kwamba, Kanisa limepata Papa Mpya baada ya Makardinali kupiga kura ya tatu, moja asubuhi iliyopelekea moshi mweusi na ile ya jioni iliyoonesha moshi mweupe.

Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro ulikuwa umeshiba watu kutoka sehemu mbali mbali za dunia waliofurika tangu asubuhi kushuhudia tukio hili la kihistoria, baada ya Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, kung'atuka kutoka madarakani kwa utashi na uhuru kamili hapo tarehe 28 Februari 2013. Wakati wowote kuanzia sasa tutakuletea jina la Papa Mpya. Tunaendelea kufanya kazi kwa ajili yako, vuta subira!







All the contents on this site are copyrighted ©.