2013-03-12 13:23:26

Sala ya waamini kwa ajili ya kuombea uchaguzi wa Papa Mpya


Waamini kutoka sehemu mbali mbali za dunia waliungana na Makardinali kwa ajili ya kusali ili kuombea uchaguzi wa Papa Mpya. Katika Sala za Waamini, wamesali kwa ajili ya kuliombea Kanisa mchumba wa Kristo, ili liweze kudumu katika ukweli, utakatifu, umoja na amani. RealAudioMP3

Mwenyezi Mungu awajalie Makardinali mapaji ya Roho Mtakatifu; awajalie akili na ushauri, hekima na mang'amuzi. Watu wote washirikiane kwa ajili ya mafao ya wengi, kwa kudumisha haki, amani, utulivu na mshikamano. Awafariji wote wanaoteseka na kudhulumiwa bila kuwasahau waliokata tamaa! Awaimarishe waamini katika utii na unyenyekevu, wajitoa sadaka na kuonesha upendo wa dhati.

Sala ya Waamini kwa Lugha ya Kiswahili kwa ajili ya kuombea mchakato wa uchaguzi wa Papa Mpya imetolewa na Sr. Martha Msambiri, kutoka Shirika la Masista wa Upendo wa Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili la Ivrea.







All the contents on this site are copyrighted ©.