2013-03-07 07:44:30

Kikao cha Nne cha Makardinali - Vatican


Kikao cha nne cha Mkutano wa Makardinali Jumatano kilianza , majira ya saa tatu na nusu, kwa masifu ya asubuhi , kukiwa na Makadinali 153, katika ujumla wao , wenye haki ya kupiga kura na wasio wapiga kura.

Katika kikao hiki, Makardinali wanne, waliowasili Jumanne jioni na asubuhi ya Jumatano, Kardinali Lehmann, Kardinali Naguib, Kardinali Tong Hong na Kardinali wetter walijiunga na wenzao. Kati yao watatu ni wapiga kura - Lehmann, Naguib na Hong Tong, na waliapa na hivyo kuifanya idadi ya Makadinali waliopo wapiga kura kuwa 113.

Na kwamba, hadi asubuhi Jumatano , Makardinali wawili walikuwa bado kuwasili, Kardinali Nycz wa Warsaw, na Mwingine kutoka Vietnam anayetarajiwa kuingia Alhamis. Hivyo kama atawasili kama ilivyopangwa, basi idadi ya Makadinali wote wenye haki ya kupiga kura itakuwa imetimia.

Pia Padre Lombardi alieleza kwamba, Dekano wa Makardinali, Kardinali Sodano, mapema alituma salaam za pongezi kwa Kardinali Kasper ambaye amedhimisha miaka 80 ya kuzaliwa. Pia salaam za matashi mema ya siku kuu ya kuzaliwa zimetolewa kwa Kardinali Coccopalmerio kwa kuadhimisha miaka 75 ya kuzaliwa Jumatano hii, Na Alhamisi slaamu hizo zitatolewa kwa Kardinali Terrazas anayetimiza miaka 77.

Msemaji wa Vatican, ameendelea kubainisha kwamba, Asubuhi kulikuwa na michango 18 iliyotolewa na Makardinali mbalimbali, kupitia utaratibu wa hotuba fupifupi, katika kikao hiki kilichohdhuriwa na Makardinali 51. Kati ya mandhari zilizo jadiliwa ni Kanisa katika ulimwengu wa leo: haja ya uinjilishaji mpya. Ingine ni Kiti Kitakatifu, Idara na uhusiano na Maaskofu.

Pia waliendelea kujadili juu ya sifa zinazo faa kwa Kardinali kuteuliwa kuwa Baba Mtakatifu, katika muono wa matarajio ya dunia na haja ya utawala bora kwa Kanisa la Ulimwengu. Hat hivyo kutokana na ufinye wa muda kila mwenye maoni alipewa muda wa dakika tano.

Na kama ilivyokuwa jana , pia leo, wakuu wa idara mbalimbali wanaohusika na utendaji wa kazi Idara pia walipewa muda wa kuzungumza na kujibu maswali yaliyoulizwa miongoni mwa mengine. Na kwamba, Alhamisi , kutakuwa na vikao viwili ,asubuhi na jioni , kwa ajili ya uimarishaji wa kasi ya kufanya kazi kwa pamoja.

Katika hatua hii, kama ilivyokuwa Jumanne, waandishi wa habari wakiwa katika Ofisi habari za Vatican, walitazama onyesho la video, lillo andaliwa na Kituo cha Televisheni Vatican. Pia walitazama onyesho la picha za kwanza katika kikanisa cha Mtakatifu Paulo, na michoro ya wongofu wa Paulo iliyochorwa na Michelangelo na Kusulibiwa wa Mtakatifu Petro. Baadaye walitazama kazi inayoendelea katika Kikanisa cha Sistine, kuelezwa jinsi itakavyoandaliwa tayari kwa ajili ya upigaji wa kura katika kikanisa hicho.








All the contents on this site are copyrighted ©.