Kikao cha Tatu cha Makadinali : hakuna tarehe iliyopangwa ya conclave.
Padre Federico Lombardi, Jumanne majira ya saa saba alitoa muhtasari kwa wanahabari
katika kile kilicho endelea katika Mkutano wa kawaida wa Makardinali kwa ajili ya
maandalizi ya Kikao cha "conclave" cha kumchagua Papa Mpya . Mkutano huo kwa
wanahabari ulifanyika katika Ofisi ya Habari ya Vatican. Padre Lombardi, alitaja mambo
muhimu yaliyofanyika kwamba, asubuhi Jumanne, Makardinali, walituma ujumbe kwa
Benedict XVI. Na kwamba bado maamuzi hayajafanyika juuya tarehe ya kuanza vikao vya
Conclave. Jumatatu jioni, Makardinali walisikiliza, tafakari ya Neno la Mungu kutoka
kwa Mhubiri katika jengo la Kipapa, Padre Raniero Cantalamessa. Padre Federico
Lombardi pia amesema, Makardinali waliofika Roma , Jumatatu jioni, ambao hawakuwepo
katika kikao cha Asubuhi, walifanya kiapo chao wakati wa kikao cha jioni, hasa wapiga
kura, Kardinali Rai, wa Upatrikai wa Lebanon ya Maronite Kardinali Meisner, Askofu
mkuu wa Cologne, Kardinali Völki, Askofu Mkuu wa Berlin, Kardinali Sarr, Askofu Mkuu
wa Dakar na pia Kardinali Duka , Askofu Mkuu wa Prague. Na jana iliamuliwa kwamba,
watakuwa na vikao wakati wa asubuhi tu kwa Jumanne na Jumatano. Jumanne asubuhi,
wakati wa Kikao cha tatu kimefanyika kati ya 9.30 na 12.40, ambamo baadhi ya Makardinali
waliowasili Jumanne, wenye haki ya kupiga kura, walikula kiapo chao. Nao ni Kardinali
Rouco Varela na Kardinali Grocholewski. Na hivyo, hadi nyakati za mchana, Makadinali
wapiga kura walikuwa 110 katika kusanyiko hilo la Makardinali 148 waliofika kwa
mkutano huo . Na kwamba, katika kikao cha tatu asubuhi, michango 11 ilitolewa
na Makadinali kwa mada za mkutano , ikwemo shughuli za Jimbo Takatifu na idara
zake mbalimbali, uhusiano wa Makardinali na Maaskofu, upya wa Kanisa katika mwanga
wa Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican, hali ya Kanisa na mahitaji ya uinjilishaji mpya
katika ulimwengu, na hali tofauti za kitamaduni. Na kwamba , katika yote, kati
ya jana na leo, kuliwakilishwa jumla ya michango ya maoni 33, kutoka mabara matano.
Na kwamba, Makadinali bado wanaona haja ya kuwa na muda zaidi wa maandalizi ya
kutosha kwa ajili ya vikao muhimu vya Conclave. Padre Lombardi anasema, hakuna sababu
za kuharakisha. Na pia alitangaza kwamba, mchana Jumatano , majira ya saa 11
za jioni, katika Madhabahu Kuu ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro , Makardinali watakusanyika
kwa ajiliya Ibada ya Kuabudu na masifu ya Jioni, wakiongozwa na Decano wa Decania
ya Makardinali , Kardinali Angelo Sodano. Makardinali kwametoa mwaliiko kwa kanisa
zima, kuungana nao wakati huo , kwa ajii ya kuiombea kazi hii muhimu ya uchaguzi
kwa Kanisa. Aidha Padre Lombardi amesema, kwa ajili ya kazi za kuandaa kikanisa
cha Sistine, kwa uchaguzi: Kikanisa hicho kimefungwa tangu leo kwa watalii na wageni.
Na hatimaye, Padre Lombardi alitoa taarifa juu ya uwepo wa vyombo vingi vya
habari, vilivyofika Roma kwa ajili ya uchaguzi huu akitaja kwamba, kuna wanahabai
karibia 4,432 wenye dhamana waliotoka mataifa 65 kwa ajili ya utoaji habari katika
lugha mbalimbali 24.