Shirikisho la Waluteri la Dunia (LWF), limetoa shukurani kwa Baba Mtakatifu Mstaafu
Benedikto XV1, kwa juhudi alizoonyesha katika kujenga mshikamano na umoja wa Wakristu
yaani uekumene , hasa katika siku za mwisho wa utawala wake. LWF, katika barua
yake iliyotiwa sahihi na Rais wa LWF, Askofu Munib Younan na Katibu Mkuu Martin Junge,
mmeandikwa , "Tumejisikia kutiwa nguvu na ahadi yake inayothamini kwa kina majadiliano
ya kiteolojia na kuekumeni , yanayolenga kuupata umoja kamili wa Kanisa hata katika
misingi ya majiundo thabiti ya miito kwenye Ushariki wa Waluteri. Viongozi hao
wametoa ahadi ya kutunza waliyo jadili katika mkutano pamoja na Papa Benedikto XV1,
hapo Desemba 2010, ambamo kwa namna ya kipekee, alisisitiza majiundo msingi ya pamoja
kati ya waluteri na Wakatoliki,na hasa tafakari za pamoja wanapotembea katika njia
ya kuelekea umoja kamii. Barua ya LWF, inaendelea kutoa shukurani kwa Papa msaatafu,
kwa jinsi alivyo liongoza Kanisa Katoliki, katika kuwa na mwendelezo wa majadiliano
juu ya Uinjilishaji mpya. juhudi hizo, zimechochea pia makanisa mengine ya Kikristu
kutafakari juu ya wajibu wao, katika kushiriki kwenye utume wa Mungu, kwenye dunia
ya sasa. Barua inaeleza, kwanza, walishtushwa na taarifa ya kustaafu kwa Papa
, lakini baada ya kutafakari kwa kina sababu za kustaafu kwake, wameona kwamba, ni
kitendo cha hekima na busara na ushupavu wa hali ya juu , kutoa maamuzi kama hayo
, kwa ajili ya manufaa ya kanisa . Ni pendo wa kina wa Papa Mstaafu kwa kanisa la
Kristu, imemalizia barua hiyo.