2013-03-02 10:37:11

Idadi ya Makardinali wanaoshiriki katika mchakato wa kumchagua Papa Mpya!


Idadi ya Makardinali wote kwa sasa ni 207, kati yao kuna Makardinali 117 ambao wana haki ya kupiga na kupigiwa kura wakati wa uchaguzi wa Khalifa wa Mtakatifu Petro. Kuna Makardinali 90 ambao wamekwisha vuka umri wa miaka 80 ambao hawana tena haki ya kupiga au kupigiwa kura. Makardinali nao pia wanatofautiana kwa vyeo vyao.

Kuna Makardinali- Maaskofu ambao kwa sasa idadi yao ni 6. Hawa ni wale ambao wamepangiwa Majimbo maalum yaliyoko mjini Roma. Kuna Makardinali-Mapadre ambao wamepewa dhamana ya utume katika baadhi ya Parokia zilizoko mjini Roma, hata kama wanaongoza Majimbo yao.

Kwa mfano Kardinali Polycarp Pengo, Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam amekabidhiwa Parokia ya Madonna delle Salette. Katika orodha ya Makardinali kuna Makardinali-Mashemasi, hawa katika historia ya Kanisa walikuwa ni wahudumu wa vitongoji mbali mbali vya mji wa Roma.







All the contents on this site are copyrighted ©.