Vuteni subira! Yesu bado anatenda miujiza ndani ya Kanisa lake!
Bila shaka waamini wengi wanalikumbuka lile tukio la Yesu kuwatetea wafuasi wake waliokuwa
wamekaa siku nzima wakimsikiliza kwa makini, alipoambiwa na Mitume kwamba, kulikuwa
kunakuchwa awape ruhusa watu waende kujitafutia chakula vijijini kwani pale palikuwa
ni uwanda na nyika tupu!
Padre Francesco Rossi de Gasper mtaalam wa Maandiko
Matakatifu anasema, Ukristo unaweza kufahamika kihistoria, lakini unamwelekeo katika
maisha ya milele kwani unapita ufahamu na mwelekeo wa kihistoria. Ni dini ambayo inajikita
katika eneo la kijiografia na muda; mambo yote haya ni muhimu sana katika kutangaza
Hbari Njema ya Wokovu, ili iweze kupenya katika mioyo na maisha ya watu wengi zaidi;
kwa kutoa kipaumbele cha kwanza na kuheshimu utu wa mwanadamu aliyeumbwa kwa sura
na mfano wa Mungu.
Jangwa linaweza kuelezwa kuwa ni kielelezo cha uwepo wa
dhambi inayoharibu bustani nzuri iliyotengenezwa na Mwenyezi Mungu katika maisha ya
mwanadamu. Yesu akawaambia wanafunzi wake si lazima waende, wapeni ninyi chakula!
Yesu akafanya muujiza kwa kuwalisha watu elfu tano, bila kuhesabu wanawake na watoto.
Yesu bado anatenda miujiza kwa ajili ya Kanisa lake! Vuteni subira!