2013-03-01 11:47:58

Vurugu za kisiasa nchini Zambia za sababisha maafa!


Heri wapatanishi maana hao wataitwa wana wa Mungu ni ujumbe kutoka kwa Baraza la Makanisa Zambia, ambalo limesikitishwa na fujo na vurugu zilizojitokeza hivi karibuni nchini Zambia kiasi cha kupelekea baadhi ya watu kupoteza maisha yao walipokuwa wanashiriki katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Livingstone.

Baraza la Makanisa Zambia lina laani vitendo vya vurugu vinavyosababishwa na masuala ya kisiasa na wanawaomba wananchi wa Zambia kuwa watulivu na kuachana na ushabiki unaoweza kusababisha maafa makubwa kwa watu wasiokuwa na hatia n chini Zambia.

Jeshi la Polisi litekeleze wajibu wake kwa kuzingatia sheria za nchi. Huu si wakati wa kutupiana lawama, bali kila upande uchunguze dhamiri na kuangalia kiwango cha kisiasa kilichofikiwa na wananchi wa Zambia na kuhoji ikiwa kama hii ndiyo njia sahihi wanayopaswa kuichukua!









All the contents on this site are copyrighted ©.