2013-03-01 09:13:34

Kardinali Jean Marcel Honore afariki dunia!


Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, Alhamisi tarehe 28 Februari 2013 ametuma salam za rambi rambi kwa Askofu mkuu Bernard- Nicolas Aubertin wa Jimbo kuu la Tours, Ufaransa kufuatia kifo cha Kardinali Jean Marcel Honore, Askofu mkuu mstaafu wa Jimbo kuu la Tours, aliyefariki dunia hapo tarehe 28 Februari 2013 akiwa na umri wa miaka 92.

Baba Mtakatifu katika salam zake za rambi rambi anasema kwamba, Kardinali Honore alikuwa ni kiongozi aliyelihudumia Kanisa kwa kujitoa bila ya kujibakiza, hasa katika sekta ya elimu na katekesi ya kina. Anaiombea roho ya Marehemu kardinali Honore iweze kupokelewa amani na mwanga wa milele. Itakumbukwa kwamba ni kati ya viongozi waliohariri Katekesimu Mpya ya Kanisa Katoliki, kwa ari na moyo mkuu akitamani daima kutangaza Injili ya Kristo hadi miisho ya dunia!







All the contents on this site are copyrighted ©.