2013-02-25 14:57:03

Jopo la Makardinali lililochunguza uvujaji wa nyaraka za siri kutoka Vatican lakutana na Papa Benedikto XVI


Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, Jumatatu, tarehe 25 Februari 2013 amekutana na Jopo la Tume ya Makardinali watatu: Julian Herranz, Joseph Tomko na Salvatore de Giorgi waliokuwa wamepewa dhamana ya kuchunguza uvujaji wa nyaraka za siri kutoka Vatican. Jopo hili liliongozana pia na Padre Luigi Martignani, O.F.M.

Baada ya kuhitimisha kazi yao, Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, amewashukuru Makardinali hawa kwa kazi kubwa waliyoifanya. Uchunguzi wao umedhihirisha udhaifu wa binadamu unaoweza kujitokeza katika taasisi yoyote ile, bila kusahau kwamba, kuna watu wengi zaidi wanaotekeleza wajibu na dhamana yao kwa ukarimu, unyofu na sadaka kubwa, kwa ajili ya huduma kwa Kanisa na kwa Khalifa wa Mtakatifu Petro.

Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita ameamua kwamba, taarifa ya uchunguzi iliyofanywa na Jopo la Tume ya Makardinali itatolewa kwa Papa Mpya peke yake!







All the contents on this site are copyrighted ©.