2013-02-23 16:51:51

Tahariri ya Padre Federico Lombardi


Katika kipindi hiki cha wiki la mwisho la Utawala wa Baba Mtakatifu Benedikto XV1, na hali ya kubaki na kiti kitupu cha Petro na maandalizi ya Papa mpya kuchaguliwa katika kikao cha Conclave,kwa wafanyakazi wa Vatican, ni kipindi cha kazi nyingi na habari nyingi.
Ni wazi si sawa na kipindi cha uchungu wa kufiwa na Papa, lakini hata kujiuzuru kwa Papa kuna kishindo chake, na hasa katika kuwa waangalifu katika kujibu maswali na habari zinazotolewa, inakuwa ni jambo la muhimu kujiepusha na mtihani mwingine na maongezeko ya mashinikizo mageni kutoka nje ya roho ya kikanisa, yanayojitokeza katika wakati huu ambamo Kanisa linapenda kuishi katika hali ya utulivu, matumaini na maandalizi ya kuchaguliwa kwa Papa mwingine. .

Hivyo katika ukweli wake kwamba, hapakosekani , wanaotafuta kunufaika na kipindi hiki cha mpito wa kuelekea uchaguzi mpya wa Papa, kutumia vyombo vya mawasiliano na habari kutoa habari za uzushi na zisizo za kweli na kashfa pia kwa lengo la kudhoofisha au kupotosha nia safi za Kanisa na Chuo cha Makardinali, katika taratibu na wajibu wake wa kumchagua mmoja wao kushika nafasi hii nyeti ya kiti cha Petro.

Pamoja na hayo , Mhariri anasema , hayo yote hayatabadili mtazamo wa waumini, wala kuathiri imani na matumaini, katika ahadi ya Bwana, kuliongoza Kanisa.
"Tunataka, kama inavyo tajwa katika mapokeo na sheria ya Kanisa, kuonyesha kwamba, huu ni wakati wa kutafakari kwa dhati juu ya matarajio ya sasa ya ulimwengu wa kiroho na uaminifu wa Kanisa na Injili, kupitia maombi kwa msaada wa Roho Mtakatifu, ili aangazie kwa ukaribu zaidi Chuo cha Makardinali, katika umoja na mshikamano wao na katika huduma , utambuzi na uchaguzi, kuwa mambo msingi katika utendaji wao kwa wakati huu.
Na ameongeza kwamba, katika wakati huu , waamini wanasonga mbele kwa kutazama mfano wa uadilifu wa kiroho wa Papa Benedict XV1, ambaye, ameutolea muda huu wa kukianza kipindi cha Kwaresima kwa sala na mafungo , kama sehemu ya mwisho ya safari yake ya kipapa. Safari ya maungamo na uongofu katika furaha ya Pasaka. Na hivyo ndivyo tutakavyokiishi kipindi hiki, cha utupu ktika kiti cha Petro, kwa hali ya uongofu na matumaini.








All the contents on this site are copyrighted ©.