2013-02-22 13:56:36

Mzee Amos Kaguta afariki dunia


Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda pamoja na familia yake wanaomboleza kifo cha Mzee Amos Kaguta, baba yake mzazi wa Rais Museveni aliyefariki dunia Ijumaa, tarehe 22 Februari 2013 akiwa na umri wa miaka 96. Mipango ya mazishi inaendelea kufanywa nyumbani kwa Mzee Amos Kaguta huko Rwachitura, Magharibi mwa Uganda, yaani kilometa mia 200 kutoka Jijini Kampala.

Familia ya Rais Museveni wa Uganda inawashukuru madaktari wa Hospitali ya Kimataifa, Kampala waliomhudumia Mzee Amos Kaguta, hadi pale Mwenyezi Mungu alipoamua kumwita mja wake kutoka bondeni huku kwenye machozi. RIP.







All the contents on this site are copyrighted ©.