2013-02-22 15:19:45

Imani na sayansi katika utetezi wa Maisha ya binadamu


Katika kilele cha Mkutano Mkuu wa 19 juu ya Imani na Maisha ya Binadamu wa Taasisi ya Kipapa kwa ajili ya Elimu ya Maisha, mkutano wa siku tatu, kwa mwaka huu umeongozwa na Mada : Imani na Maisha ya binadamu katika sayansi.

Katibu Mratibu wa Taasisi hiyo, Padre Scott Borgman, akizungumza na Redio Vatican , alieleza kwamba, Taasisi hiyo , ni nafasi ya kufanya gunduzi na tafakari makini juu ya thamani ya maisha ya binadamu katika dunia ya leo. Na ni chombo si tu kwa manufaa ya Vatican lakini kwa kanisa lote la ulimwengu, na dunia kwa ujumla.

Katika maelezo yake, kwanza kabisa alikanusha dhania kwamba taasisi hiyo imejaa Mapadre na maofisa wa Vatican. Bali ni chombo cha wanasayansi na wasomi watalaam ambao hujikita katika kuchambua hoja zinazowaka moto leo hii, kama vile haki ya maisha, jenda, na utetezi wa maisha na familia , katika kutaja machache.

Na kwamba, katika mikutano yao kuna mapadre au makreli wachache, na hivyo wengi wao ni walei wanaofanyakazi katika hospitali mbalimbali na taasisi nyingine za kisayansi duniani. Kwa mkutano huu wa Roma ulikamilika ulihudhuriwa na wajumbe 120, walio shiriki kuichambua mada ya Mkutano ya mwaka huu: Imani na maisha ya binadamu.
Katika mada hii, washiriki wa Mkutano wamelenga zadi katika Kanisa na Maandiko Matakatifu, yanavyo tufundisha juu ya asili ya maisha ndani ya familia iliyosimikwa katika misingi ya maisha ya ndoa kati ya mwanamme na mwanamke.
Askofu Mkuu Muller, Mkuu wa Shirika la Mafundisho Sadikifu, amezungumzia juu ya maisha ya binadamu kwa mujibu wa mafundisho ya Kanisa na msingi wa utendaji wote wa kibiolojia na tiba , katika kuheshimu maisha ya kila biandamu na pia asili ya maisha ya binadamu katika ndoa ya mke na mme na familia.
Mwaka jana, kati ya mengine mkutano ulizungumzia tatizo la ugumba , na matumizi ya kondo la binadamu katika maabara.








All the contents on this site are copyrighted ©.