2013-02-21 15:43:09

Jamii ya Kisasa , inaunda miji yenye watu wengi wapweke- Kardinali Ravasi


Maumivu na kutengwa ni kiini cha tafakari ya Kardinali Gianfranco Ravasi, kwa Papa na wafanyakazi katika jengo la Kipapa na Curia ya Roma kwa siku ya Jumatano mchana, walipokuwa wakiendelea na zoezi la kiroho la kipindi cha Kwaresima. Kwa kifupi alisema, Jamii ya kisasa imeunda katika miji, umati wa watu wapweke na wateswa.
Kardinali Ravasi aliendelea kuitazama sura ya Kristu aliyemwilisha, katika sura ya mtu mteswa na mpweke. Na kwamba, mbele ya mateso, binadamu hukosa jibu , na hivyo huweza kukata tamaa au kuishi katika hali ya ukimya na upweke. Kardinali alieleza na kurejea uzoefu wa mwanafalsafa Emmanuel Mounier Mfaransa, ambaye mbele ya mateso ya maradhi ya binti yake aliyekuwa akisumbuliwa na uvimbe ndani ya ubongo, aliyeita maradhi hayo kuwa ni fumbo au siri kubwa, katika picha ya imani.
Kardinali alieleza na kutaja umuhimu wa huduma kwa wanaoteseka, akirejea maelezo mengi ya mzaburi, kuhusu maradhi, maumivu, machozi, ndoto ya kifo, upweke, kutelekezwa na marafiki wa zamani. Mzaburi anaonyesha kwamba, katika hali hizi zote Mungu bado karibu. Hata kama marafiki wameniacha mimi – Yeye kamwe hataniacha. Bwana, anasikia maombi yangu, Bwana anapokea maombi yangu.

Aliendelea kuainisha aina mbalimbali za mateso, na kutoa ufafanuzi juu ya mateso ya wale ambao wametengwa na kuwekwa katika majaribu ya kuulizwa , "Yuko wapi Mungu wako?" Lakini Mzaburi anasema, Mungu hatakuacha, na kule tu kule kufikiri kwamba Munguyupo karibu nami ni faraja kubwa. Ameeleza mateso ya kutengwa Kutengwa, ni uwanja wa mawindo ya shetani kama alivyoandika mwandishi Mrusi, au kutelekezwa kuwa ni janga la dunia ya kisasa, na mtihani mkubwa kwa wanaomfuata Kristu. .

Kardinali ameeleza na kuangalisha fikira, katika miji mikubwa, ambako kuna maelfu ya maelfu ya watu wapweke wanao subiri hodi kupigwa mlangoni, walao wapate neno la faraja , lakini hakuna hata anayejitokeza . Siku zote hubaki kimya katika majengo hayo makubwa ya ghorofa, jamii ikiendelea na shughuli zake bila ya kujali hata kama kuna binadamu anayeishi kando yao kwenye ghorofa moja.

Amesema, inashangaza kuona haya yakitokea katika dunia yetu pia maovu ya mmoja kumharibu mwingine kwa makusudi, akitolea mfano wa uchungu wa masingizio yanayochoma moyo kama misumari na kumwingiza mtu katika upweke na kujitenga. Kardinali, ametaja hili kwa kuwakumbuka wahanga wa uonevu unaofanywa sasa katika mitandao au online, ambamo vijana, wamekuwa na mchezo wa kufanya kejeli kdhdi ya wenzao, na kusababisha madhara makubwa hadi mtu kuona heri kufa kuliko kuendelea kuishi.
Ameasa, haifai kusema, Mungu anawaona, na kujiweka mbali na wenye shida na wahitaji, kwa mfano watoto wanaoteswa na njaa barani Afrika au Asia. Au iwapo tunafahamu uwepo wa mipango ya watu wadhalimu kutka kushambulia wengine kw amabomu ya kuua, watu wasiokuwa na hatia kama watoto. Kwa namna hiyo pia alitazama mateso ya watot wanaodhulumiwa kijinsia na watu wazima, akisema, watu wazima wanapaswa kuwa kioo cha masiha bora kwa watoto.







All the contents on this site are copyrighted ©.