Marehemu Padre Evarist Mushi, wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph la mjini Magharibi
Zanzibar aliyeuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana Zanzibar Jumapili iliyopita,
Jumatano hii amezikwa kwa heshima kubwa. Ibada ya Misa ya wafu iliyosomwa kwa nia
ya kumwombea Marehemu ilifanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Josef la Minara Miwili,
Zanzibar. Viongozi mbalimbali wa Kanisa na kijamii wamehudhuria mazishi haya,
akiwemo Rais wa Zanzibar , Dr Al Mohamed Shein, viongozi wengine wa ngazi za juu
wa vyama vya kisiasa na kijamii, na uwakilishi mkubwa kutoka viongozi mbalimbali
wa makanisa mengine kama KKKT, Anglican, Pentecoste na jumuiya za kikanisa. Askofu
Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, aliongoza
Ibada ya Misa ya Wafu, akisaidiana na Askofu Mkuu Paulo Ruzoka wa Jimbo Kuu la Tabora,
na Askofu Tarcisio Ngararakumtwa, wa Jimbo la Iringa na Rais wa Baraza la Maaskofu
Katoliki Tanzania(TEC) . Marehemu Padre Evaristi Mushi aliuawa kwa kupigwa risasi
na watu wasiojulikani wakati akiwa katika harakati za kwenda kuadhimisha Misa katika
kanisa lake. Askofu Augostine Shayo, wa Jimbo la Zanzibar, akieleza kwa nini wameamua
Padre Mushi aliyeuawa akiwa na umri wa miaka 55, azikwe Zanzibar badala ya kwao Moshi
ameeleza kwamba, Padre Evaristi , ameishi Zanzibar tangu akiwa na umri wa miaka kumi
na nane na hivyo ni mkazi wa Zanzibar, na amezikwa katika kiunga cha Kitope. Taarifa
zinabaini , katika ukweli wake, pamoja na viongozi wa serikali kukemea maovu na chuki
za kidini dhidi ya Wakristu, siku tatu tu baada ya kuuawa kwa Padre Evarist Mushi,
Kanisa la The Pool of Siloam la Zanzibar, lilichomwa moto na watu wasiojulkana na
kuharibu i zake kuharibiwa. Naibu Kamisheni wa Polisi , Yusuf Ilembo, amenukuliwa
na vyombo vya habari, akithbitisha uwepo wa tukio hilo la kusikitisha, ambalo limeongeza
maumivu katiak vidonda vingine vya uhalifu kama huo. Anasema, tukio hilo lilitokea
jana majira ya saa kumi za usiku kuamkia Jumanne, katika wilaya ya kati Mkoa wa Kusini
Unguja. Na Mkuu w Polisi nchini Tanzania, ametoa amewaonya wote wanaohusika na madhulumu
haya kwamba , kwa hakika watawajibika kwa mujibu wa sheria za nchi.