Maoni mbalimbali ya Makardinali juu ya Kjiuzuru kwa Papa Benedikto XV1
Viongozi wa Kanisa wa ngazi za juu , wanaendelea kutoa maoni yao juu ya maamuzi ya
Papa Benedikto XV1, kujiuzuru hapo tarehe 28 Feburari 2013. Kardinali Julian Herranz,
Mtaalam wa sheria za Kanisa, akitoa maoni yake anasema, kwanza alipata mshituko mkubwa
wakati Papa akitangaza maamuzi yake. Lakini mara, alipata hisia tofauti , hisia ya
furaha ndani mwake, kwa unyenyekevu na upendo, ulionyeshwa Papa kwa Kanisa . Kardinali
Herranz alieleza hayo wakati akizungumzia kustaafu kwa Papa katika mahojiano na gazeti
la El Paris , na kuchapishwa siku ya Jumanne. Alisema, kibinadamu , mara baada ya
kusikia maamuzi ya Papa alipatwa na hisia hizi za kusikitika, hasa alipotupa fikira
zake katika miaka ya nyuma, wakati alipofanya kazi bega kwa bega na Josef Ratizinger
kablaya kuwa Papa.
Na amemshuhudia kwamba, Papa Benedikto XV1, si tu mtaalum
mkubwa teolojia, lakini pia ni mtu mwenye kuwa na imani kubwa isyokuwa ya kawaida
kwa Kristu, imani anayopenda kuifikisha kwa watu wote , kwa unyenyekevu, na hivyo
si tu kupitia nguvu za mamlaka siku zote, lakini pia katika maisha ya kawaida.
Na
kama Mwanasheria anasema, maamuzi ya Papa yamefanyika kwa mujibu wa sheria ya kanisa
namba 332, kipingere cha 2. Hivyo Papa hajaenda nje ya sheria za Kanisa, kama wengine
wanavyofikiri. .
Na Kardinali Jean-Louis Tauran, katika mahojiano na Antoine-Marie
Izoard wa gazeti la "Insider Vatican," alielezea zaidi juhudi zinazofanywa na Papa
katika siku za hivi karibuni katika kwenda sambamba na kishindo cha mawasiliano jamiii.Amesifu
kwamba, juhudi hizo, zimewezesha wengi kutazama kwa makini zaidi, jinsi ya kukabiliana
na changamoto kubwa katika dunia ya kisasa. Pamoja na uchaguzi wake - aliongeza -
ametuonyesha jambo lisilokuwa la kawaida la uwepo wa nguvu ya ndani isiyokuwa na kipimo.
Nae Askofu Mkuu Christoph Schönborn, Austria katika gazeti la Austria la "Profil"
akinukuliwa pia na gazeti la "Corriere della Sera" matoleo ya Februari 19, anasema
kujiuzuru kwa Josef Ratzinger, kuonyesha kwamba, katika mwamba ambayo Kristo amejengwa
Kanisa lake, pia bado una utendaji wa mtu binafsi katika maamuzi yake kwa manufaa
ya kanisa na ofisi ya Papa" Na tena: Haya ni maamuzi ya dhamiri na uchaguzi binafsi
wa Ratzinger, alioufanya kwa mujibu wa sheria ya Kanisa ya mwaka 1917." Kardinali
Donald Wuerl, Askofu Mkuu wa Washington, pia ameiambia Redio Vatican kwamba, Kujiuzuru
kwa Papa kumezingatia mahitaji ya “Papa katika nyakati hizi za Kisasa ambamo Papa
anatakiwa pia kuwa na ratiba nyingi za kusafiri hapa na pale, kwa ajili ya kuimarisha
waamini katiak maeneo mengi zaidi duniani. Na hivyo kwa busara na hekima Papa Benedikto
XV1, ameona haNa tena nguvu za kufanya hivyo , badala ya kung'ang'ania anaona umefika
wakati wa mtu mwingine ambaye anauwezo zaidi kimwili kusonga mbele ratiba muhimu
za Kanisa la Ulimwengu.
Pia Kardinali Emmanuel Wamala, Mstaafu Askofu Mkuu
wa Kampala Uganda , amesema kuwa, sote tunapaswa kuheshimu maamuzi yake, na kumwombea,
kama yeye anavyoahidi kutuombea pia.