2013-02-20 10:58:26

Jumuiya ya Kimataifa kushuhudia utiaji mkataba wa amani nchini DRC hapo tarehe 24 Februari 2013


Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Ban Ki-Moon anatarajiwa kuhudhuria kwenye tukio la kihistoria la utiaji wa sahihi kwenye mkataba wa kusitisha vita ya wenyewe kwa wenyewe nchini DRC hapo tarehe 24 Februari 2013. Umoja wa Mataifa unapenda kushiriki kikamilifu kwa kutoa vikosi vya ulinzi na usalama pamoja na nchi jirani kusitisha hifadhi kwa vikosi vya waasi, kikundi au mtu anayetuhumiwa kuleta machafuko nchini DRC.

Mkataba huu unaungwa mkono na nchi za DRC, Rwanda, Burundi, Uganda, Angola, Tanzania, Jamhuri ya Afrika ya Kati pamoja na Afrika ya Kusini. Umoja wa Mataifa utakuwa ni vikosi vyenye wanajeshi 2,500 kwa ajili ya kudhibiti Kikundi cha M23, ambacho mwaka 2012 kilianzisha mapigano mapya Kaskazini mwa Kivu, kwa kushirikiana na vikosi vingine vya waasi wa Serikali ya DRC.

Wachunguzi wa mambo wanasema, hali ya ulinzi na usalama nchini DRC bado ni tete, kuna uwezekano mkubwa kwamba, mkataba huu ukashindwa kutekelezwa kama inavyokusudiwa na Jumuiya ya Kimataifa.







All the contents on this site are copyrighted ©.