2013-02-19 15:44:56

Kujiuzuru kwa Papa Benedikto ni funzo kubwa kwa dunia- Kardinali Comastri.


Kardinali Angelo Comastri, Msimamizi Mkuu wa Utawala wa Jiji la Vatican na Padre Mkuu wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, akiieleza hali halisi baada ya Papa Benedikto XV1, kutangaza maamuzi yake ya kustaafu mwishoni mwa mwezi huu anasema, kama ilivyokuwa kwa watu wengi, pia yeye , mara alipokea maamuzi ya Papa kwa huzuni kubwa na mshangao na kuingiwa na hofu na wasiwasi.
Lakini baada ya kufikiri kwa makini zaidi , alianza kufunuliwa taratibu na kuupata ujumbe wa Papa kujiuzuru, aksikia kama upepo mwanana unaotoka mbali, kama harufu nzuri ya inayotoka katika majani ya Bethlehemu. Harufu nzuri ya unyenyekevu wa Mungu katika nyakati hizi, licha ya kupitia kwa historia ya miaka 2000 ya kanisa, maneno ya Kanisa yanaendelea kusikika upya kama vile yamenenwa sasa, na yataendelea kuwepo katika mishipa ya Kanisa, maneno yasemayo “Jifunzeni kutoka kwangu , maana mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo”.

Kardinali Comastri analinganisha maneno hayo na kujiuzuru kwa Papa akisema , yamemekuwa ni faraja kubwa katika kugundua na kuipata sura yna maana ya kujiuzuru kwa Papa Benedikto XVI, kwamba, ni ushuhuda na somo kubwa kwa kila mmoja, na hasa kwa viongozi. Na hasa katika dunia ya nyakati hizi ambamo watu wengi wamemezwa na moyo wa kutaka kupanda madarakani na kuendelea na hamu ya kutaka kupanda juu zaidi na zaidi, kinyume na Injili.
Hivyo maamuzi ya Papa , yamekuwa ni ishara kuu ya unyenyekevu wa kiinjili, kujiweka katika mikono ya Bwana na kusema kwa uaminifu, nisamehe mimi, kwa kuwa sina tena nguvu. Ni kumwita Yesu kwa mara ingine na kusema , Bwana nilihusu nijiondoa taratibu kwa hiari, ili nijiweka katika ukimya na sala.
Kwa hayo Kardinali Comastri anaona maamuzi ya Papa Benedikto XV1, kuwa ni Unyenyekevu wa hali ya juu na ushupavu . "Asante, Papa Benedict! Umetoa pigo kubwa kwa kiburi cha wote duniani. Maamuzi yako yameishangaza dunia nzima na kuliinua Kanisa. Na sisi sote, tumeitwa kuwajibika mbele za Mungu kwa tabasamu kwa sababu ya miari ya mwanga ulioutoa katika kufuta ukungu mnene wa kiburi cha binadamu. Na Kanisa linaendelea safari yake, endelevu na uhakika kwamba Yesu ni kiongozi wake, na hilo latosha kutufanya Kanisa kuendelea katika tumaini".

Kardinali Comastri pia, akijibu swali ju ya urithi unaoachwa na Papa Benedict XV1, anasema, ni himizo la kuendele kuisoma historia ya Kanisa, kama jambo la mwendelezo, na si kuisoma katika mtazamo wa vipandevipande, kama ilivyo kwa wengi. Mafundisho ya Benedikto XV1, yanasema, hakuna, vipande vipande katika Kanisa, bali matukio yote ni mwendelezo wa historia ya Kanisa. Na Miaka elfu mbili wa historia ni miaka elfu mbili ya historia ya jamii ambayo ni hai na thabiti, ikilnywesha kwa maji yanayotoka chemichemi ya uzima uliotolewa na Yesu Kristu.
Papa Benedict ametupa maono muhimu sana ya kiroho ya katika kipindi cha miaka minane ya utawala wake wa Kipapa. Amefanya mengi katika kurejesha kumbukumbu za Kiinjili, sio tu kuongoza kanisa kulingana na hali halisi za mitindo ya kisiasa lakini katika kuutafuta utakatifu, na uaminifu wa Injili na kisha kujitakasa na kuondoa vumbi lote la karne zilizopita, lililingia katika uso wa Kanisa. Na kwamba ujana wa Kanisa, una nguvu kubwa ya kuondoa vumbi hili na kupata uso mpya wa Pentekoste.
Kardinali Comastri anasema, atamkumbuka Papa Benedikto XV1, kuwa Baba Mwema, Baba Mwenye hamu ya kulifikisha neno la Mungu kwa watu wwote, kwa moyo thabiti wa imani, lakini kwa unyenyekevu.










All the contents on this site are copyrighted ©.