2013-02-19 15:01:49

Baba Mtakatifu katika ukimya wa mafungo ya Kwaresima - Ibada za Kiliturujia ni wakati wa kukutana na Mungu.


Baba Mtakatifu, wasaidizi wake na watumishi wa Curia ya Roma, wako katika wiki la mafungo ya Kwaresima hadi siku ya Jumamosi wiki hii. Kardinali Gianfranco Ravasi , Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Utamaduni , ndiye Mhubiri katika mafungo haya yanayo ongozwa na Mada: Sura ya Mungu na Sura ya Muumini katika maombi.
Mapema asubuhi siku ya Jumatatu , Mhubiri alitafakari umuhimu wa Ibada za Kiliturujia, akisema ni Liturujia huwasilisha Ukuu wa Mungu..ni Epifania kuu ya Mungu..
Alitazamisha kwa kina juu ya ufunuo wa Mungu katika Neno na kama Muumbaji, akivitazama kwa makini vyote vilivyoumbwa na Mwenyezi Mungu, tangu mifumo ya sayari za ulimwenguni , nchi na milima yake na hekalu, mahali ambamo binadamu hukutana na Mungu, kupitia maadhimisho ya kiliturujia.

Aliendelea kutafakari kwa makini liturujia ya muumini na kutoa maelezo kwamba ni kuendelea kutazama uwezo wa Mungu na Kristo, katika Neno lake, linalopita uwezo wote wa binadamu, na kwa upande mwingine pia ni jicho linaloitazama sura ya jirani.

Kardinali Ravasi, alisistiza umuhimu wa uwepo wa uwiano kati ya utakatifu na utendaji katika maadhimisho Ibada za kiliturujia, akisema , vinginevyo kuna hatari ya kuwa na mwisho unaoelemea upande mmoja, na kusahau mwingine, na hasa hatari ya mikusanyiko ya watu kwa ajili ya Liturujia kugeuzwa mihadhara ya kibinadamu. Alifafanua uwiano huo kwa kurejea Maandiko Matakatifu katika Kitabu cha Isaya, kwamba sadaka na uvumba batili ni chukizo kwa Mungu. "Jiosheni na kujitakasa , Ondoeni uovu wa matendo yenu mbele za Macho ya Mungu, acheni kutenda mabaya ,bali jifunzeni kutenda mema , takeni hukumu ya haki , wasaidieni walioonewa ,wapatieni yatima haki yao na wateteeni wajane".
Hivyo Upendo, Udugu na kukiri dhambi, yanakuwa ni vipengere muhimu vya kujitafiti binafsi, wakati wa kushiriki katika Ibada ya Bwana na hasa wakati wa kukivuka kizingiti katika njia inayoongoza katika usharika na Bwana. Kwenda katika Meza ya Bwana, – kupokea moja mkate, kukinywea kikombe kimoja - na kuwa mwili mmoja, sharti la kujenga umoja thabiti na Bwana.

Kardinali aliendelea kueleza umuhimu wa kukutana na Mungu katika Ekaristi , hekalu jipya, hasa katika jamii ya nyakati hizi ambamo wengi wamemezwa na maovu na maadili kushushwa na hiari za chaguzi. Na hivyo inakuwa ni jambo la muhimu zaidi, kushuhudia mema yanayopatika katika uzoefu wa kukutana na Mungu, katika kuwa na nguvu mpya katika maisha safi.
Kardinali alihitimisha tafakari yake kumtazama Nabii zefania , ambaye anaizungumzia Sioni kama Mji- Mama unaoonyesha sura ya Kimama ya Bikira Maria “Hekalu la Mungu “ kama alivyosema pia Mtakatifu Ambrose. Sura ya umama wa Sayuni, kwa hiyo,inatwaa umbile zima la Zaburi 87, ambalo ni Kanisa lake Kristu.
Karidnali Ravasi katika mazoezi haya ya kiroho ya Jumatatu asubuhi, ambamo alitoa tafakari yake ya pili, alizama katika ufunuo wa Mungu kama Muumba na kuainisha maneno ya ufunuo wa Agano la Kale na Jipya katika mtazamo wa alama za haki za Neno la Mungu.








All the contents on this site are copyrighted ©.