2013-02-18 15:34:24

Waamini waendelea kuenzi Maamuzi ya Papa Benedikto XV1. Maoni yaendelea kutolewa juu ya kustaafu kwa Papa Bendikto XVI


Jumapili, Katika Jimbo la Roma Makanisa yote Katoliki, yalitolea sala maalum ya waumini kwa nia ya kumwombea Papa Benedikto XV1. Sala hiyo ilitishwa na Kardinali Agostino Vallini, Vika wa Jimbo la Roma, akiitaja kuwa ni ishara ya shukrani kwa Askofu wa Jimbo la Roma , ambaye ni Papa Mwenyewe Benedikto XV1, anayestaafu kuliongoza Jimbo hilo.
Padre Giuseppe Midli , Mkurugenzi wa Ofisi ya Liturujia katika Vikariati ya Roma, ameieleza nia hii iliyoombwa na Makardinali na Maaskofu wasaidizi wa Jimbo la Roma, kwamba ni kujibu kwa hamu ya wengi, walioomba kuoneysha ukaribu na mapenzi yao katika ushirika wa kiroho na sala, kwa askofu wao wa Roma anayestaafu. Na hivyo waliamua kuwa na sala hii katika makanisa yote wakati wa Ibada za Misa ya Jumapili, katika Jimbo lote la Roma.

Kardinali Vallini ameendelea kueleza kwamba, ilikuwa ni muhimu kufanya hivyo kwa kuwa Papa Benedict XVI, amekuwa ni mfano wa kuigwa na wote, katika uwezo wa kukabiliana na hali za kila siku, uwezo wa mtu kichambua hali yake binafsi, na kuitikia sauti ya ndani kikamilifu na kwa uangalifu.
................................................................................................................................
Na Mchungaji Dr Olav Fykse Tveit, Katibu Mkuu wa Baraza la Makanisa Geneva, akirejea kustaafu kwa Papa Benedikto XV1, anasema hakuna shaka maamuzi ya Papa ni ya busara na hekima. Na hivyo yanapokelewa kwa heshima zote. "Hakuna shaka maamuzi haya ni ya busara, kwa kuwa kila binadamu ana paswa kuona ukomo wake na kufanya maamuzi yake kishupavu".
Na kwamba, Kazi alizozifanya Papa katika kipindi alichokalia Kiti cha Petro, zitaendelea kuheshimiwa, na ni muhimu katika nyakati hizi ngumu kwa kanisa.
Mchugaji Tveit, anaendelea kuutazama mchango wa Papa Benedikto XV1, katika kukuza umoja wa Wakristu, na kueleza kwamba, ingawa hakuna hatua kubwa sana zilizopigwa mbele katika kipindi cha utawala wake , Yeye mwenyewe Papa, amekuwa na mtazamo mzuri wa Makanisa kuenzi ushirikiano kiekumeni, na hasa kupia njia za majadiliano na maridhiano zaidi.
Mchungaji Olav, pia ametoa ujumbe kwa yeyote atakayechaguliwa kukalia kiti cha Petro, kutenda kwa utambauzi kwamba, dunia inahitaji makanisa, kuongoza katika kutenda fadhila na wema, kwa manufaa ya wote. Ni kuihudumia dunia kwa mtazamo wa umoja kwa ajili ya kufanikisha haki na amani na maridhiano miongoni mwa jamii, katika utofauti wao wa kimbali, kitaifa , kikabila kidini n.k Ni kushupalia taratibu zinazo elekeza Wakristu kujenga umoja ulio thabiti zaidi katika kumshuhudia Kristu.








All the contents on this site are copyrighted ©.