2013-02-18 15:16:02

Maelfu ya watu wajiandikisha kushirikia Katekesi ya mwisho ya Benedikto XVI.


Hadi Jumapili , zaidi ya watu thelathini na tano efu(35), walikuwa wamejiandikisha kuhudhuria Katekesi ya Papa ya wiki ijayo, 27 Februari 2013 ambayo itakuwa ni Katekesi yake ya mwisho kwa Papa Benedikto XV1. .
Padre Federico Lombardi akizungumza na wanahabari amesema, siku hiyo , haitakuwa na utaratibu wa kawaida wa Papa kutoa Katekesi, ila Papa atakutana na watu katika utaratibu wa maadhimisho Liturujia ya Neno na sherehe ya Kipapa.
Na kwamba, tarehe 28 Februari 2013, Kituo cha Televisheni cha Vatican , kitakuwa na onyesho hai, wakati Papa atakapokuwa anaondoka katika Jengo la Kipapa, baada ya kuagana rasmi na dekania ya Makardinali. Na kwamba kwa kipiindi kisichozidi miezi miwili, atakuwa katika Makao ya Kipapa ya Castel Gandolfo, hadi hapo shughuli ndani ya Vatican zitakapokuwa zimerejea katika hali yake ya kawaida, baada ya kuchaguliwa Papa Mpya.
Aidha Padre Federico Lombardi amesema , wakati huu wa wiki moja la mafungo ya kwaresima kwa Papa na wasiadizi wake, ingawa Papa ameahirisha mikutano na mi hadhara, bado ataweka sahihi katika nyaraka zinazo husika na maisha ya kikanisa, zitakazo wasilishwa kwake na Katibu wake, Askofu Mkuu George Ganswein .
Na kwamba, Msimamizi wa kipindi cha utupu katika Kiti cha Petro, anayejulikana kwa jina la Camerlengo , Kardinali Tarcisio Bertone, tayari anafanyakazi kwa kushirikiana na wengine , kuchua hatua zinazotakiwa kufanyika wakati wa utupu katika kiti cha Petro, kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi wa Papa mpya kwa mujibu wa Katiba ya Kanisa “Universi Dominici Gregis”.
Na kwamba, tarehe ya uwezekano wa kufanyika kwa Baraza la Makardinali “conclave”kwa ajili ya kumchagua Papa , bado haijajulikana. Tarehe hiyo itapangwa kwa maamuzi ya Camerlengo, na Dekania yenyewe ya Makardinali , ikitegemea jinsi wajumbe wake 209 watakavyo wahi kufika Roma, kwa ajlli ya "conclave".








All the contents on this site are copyrighted ©.