Jumapili maelfu ya watu alimiminika katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro,
kusali sala ya Malaika wa Bwana pamoja na Baba Mtakatifu Benedikto XV1, katika kukianza
kipindi cha Kwaresima.
Papa akihutubia kutokea dirisha la chumba chake cha
kujisomea katika jengo la Kipapa, aliwasisitiza waamini katika kipindi hiki cha kwaresima
, ambamo Mama Kanisa anaadhimisha Mwaka wa Imani, kwamba ni wakati muafaka wa kugundua
upya imani kwa Mungu, kuwa ni kigezo msingi katika maisha yetu na maisha ya kanisa.
Papa aliendelea kwamba , hiii inamanisha ni mapambano ya kiroho, kwa sababu
roho wa ibilisi ambaye yu kinyume na utakatifu wetu, daima hutafuta kutuweka nje ya
maisha ya Matakatifu ya Kimungu yaliyondaliwa kwa ajili yetu. Hivyo kwa ajili hiyo
Kanisa daima katika Jumapili ya kwanza ya Kwaresima, hurejea somo la Injili, la
Yesu alivyojaribiwa Jangwani na Ibilisi wakati wa siku 40 za mafungo.
Papa
alieleza , Ibilisi ni mwerevu, hatushinikizi moja kwa moja kutenda maovu, lakini
kwa hira huyaingilia maisha yetu na vishawishi vya mambo mazuri bandia, yanayoweza
kuonekana kama ni muhimu kwa wakati huo na kumbe ni mtengo wa kwenda kinyume na imani
kwa Mungu .
Papa amesema, katika muda muhimu wa kutoa maamuzi katika maisha,
mtu anapaswa kuwa makini sana , maana ni sawa na kusimama katika njia panda au uchague
njia hii au njia ile. Ni kuchagua au kuzifuata nia binafsi, au kuisikiliza sauti ya
Mungu.
Papa alieleza na kutolea maombi kwa Mungu akisema , leo hii tunapo
tafakari Yesu jangwani, ambako alikwenda kufunga na kusali, na pia anajaribiwa na
iIbilisi, pia kwetu unakuwa ni wakati wa kukianza kipindi cha kwaresima, tukiwa tumeungana
pamoja , kuomba msaada wa Mungu, utuimarishe katika kupambana na madhaifu yetu.
Papa
pia aliutumia muda huo, kutoa shukurani zake za dhati kwa waumini wote kwa sala na
faraja walizozionyesha tangu alipotangaza nia yake ya kustaafu Kiti cha Petro, ambacho
atakiachia rasmi wiki ijayo tarehe 28 Februari 2013.