Vatican na Serikali ya Italia watia sahihi katika itifaki ya matumizi ya viunga vya
mji wa Roma
Serikali ya Italia kupitia Wizara ya Utamaduni na Mambo ya Kale pamoja na Vatican,
tarehe 14 Februari 2013 wametiliana sahii Itifaki ya matumizi ya mtaa unaojulikana
kama "Passetto di Borgo na ule wa Torrino" kama njia ya ushirikiano wa dhati unaopania
kulinda na kuendeleza urithi wa kihistoria, kitamaduni na mambo ya kale.
Lengo
ni kuwawezesha watu kutembelea maeneo haya kwa kuzingatia pia mahitaji ya watu wenye
ulemavu. Baada ya ukarabati mkubwa, Serikali ya Italia itafungua tena kiunga hiki,
ili watu waweze kupata nafasi ya kutembelea Makumbusho ya Kitaifa yaliyoko "Castel
Sant'Angelo".
Itifaki hii imetiwa sahihi na Kardinali Giuseppe Bertello, Rais
wa utawala wa Mji wa Vatican pamoja na Professa Lorenzo Orhaghi, Waziri wa Utamaduni
na Mambo ya Kale nchini Italia na kushuhudiwa na viongozi waandamizi kutoka pande
zote mbili.