2013-02-12 08:29:48

Kanisa kuwatangaza watakatifu wapya watatu hapo tarehe 12 Mei 2013


Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita katika mkutano maalum na Dekania ya Makardinali hapo tarehe 11 Februari 2013 ameridhiwa Wenyeheri wafuatao kutangazwa kuwa watakatifu hapo tarehe 12 Mei 2013.

1. Mwenyeheri Antonio Primaldo na Wenzake: wafiadini.
2. Laura wa Mtakatifu Catherina wa Siena Montoya y Upegui, Bikira na Mwanzilishi wa Shirika la Masista Wamissionari wa Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili na Shirika la Mtakatifu Catherina wa Siena.
3. Maria Guadalupe garcia Zavala, Mwanzilishi mwenza wa Shirika la Wahudumu wa Mtakatifu Margharita Maria wa Maskini.

Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, aliungana na Makardinali 51 kwa kusali pamoja Sala ya Kanisa pamoja na kutoa mahubiri mafupi. Baada ya kupata maelezo ya kina kuhusu Wenyeheri hawa kutoka kwa Kardinali Angelo Amato, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa linaloshughulikia kuwatangaza waamini kuwa wenyeheri na watakatifu, aliuliza maoni ya Makardinali nao wakakubali, ili waweze kutangazwa na kuandikwa kwenye Orodha ya Majina ya Watakatifu wa Kanisa Katoliki.







All the contents on this site are copyrighted ©.