Tahariri: Vijana katika ulimwengu wa tamaduni nyingi
Kwa Jinsi gani tunaweza kuelewa hisia, fikira,na namna ya kujieleza kwa vijana? Amehoji
Padre Federico Lombardi katika tahariri yake ya wiki hii , na kutoa jibu kwamba ni
vigumu, kwa sababu ya upeo wa macho ya leo,unazidi kukanganyikiwa na mabadiliko
ya haraka sana, mabadiliko ya kiakili, mila, tabia. Na ndivyo ilivyo , kama alivyosema
Papa ,hali hiyo, ni utamaduni ulioenea ulimwenguni kote, kwa lugha nyingi tofauti
zinazoonekana katika tabia, sifa na wingi wa maono na mitazamo.
Na hivyo kutokana
na ugumu huu, Baraza la Kipapa kwa ajili ya Utamaduni, linaona haja ya kidharura,
kutafakari juu tamaduni za vijana. Jitihada zinazotafutwa ni kukazia utoaji
wa majibu sahihi katika maswali msingi na muhimu katika haja za vijana. Ni kutoa
majibu ya kueleweka, katika lugha nyepesi na mbinu zenye mikakati ya kuweza kuifikia
au kuigusa mioyo na akili za vijana, kama walivyo. Padre Federiko Lombardi anaendelea
kuzitazama haja za vijana, hata katika ulimwengu wa tarakimu(digital) na muziki wa
pop au rock, akisema yote hayo yanaweza yasikidhi majibu yetu. Kwa kuwa hhayo haitoshi,
kupata jibu sahihi, kunatoa hoja ya kushirikiana na vijana kwa ukaribu zaidi, kuwapenda
na kuwa na imani nao kama alivyoeleza Baba Mtakatifu. Ni kushirikianao nao bega ka
bega katika uchambuzi wa kulipata jibu linalowafaa na kuwasadikisha kwamba wao ni
watu wazima wa kesho. Na kwamba ndani ya Kanisa, daima kuna waelimishaji wengi
wa ajabu na marafiki wa kweli wa Vijana, ambao wanaweza kuwa msaada mkubwa kwa vijana
kupata jibu linalofaa linalotafutwa na vijana. Kanisa daima haliwakatishi tamaa au
kuwapuuza vijana, badala yake katika nyakati zote hutafuta kutembea na vijana katika
maisha yao kwa ajili ya kuipata maana ya kweli ya maisha.