Baba Mtakatifu Benedict XVI, Ijumaa aliendeleza jadi yake ya kila mwaka kutembelea
Seminari Kuu ya Jimbo la Roma, katika kuiadhimisha Siku Kuu ya Kiliturujia ya Mama
yetu wa Matumaini. Akiwa katika seminari hiyo, alionyesha kufurahia wingi wa vijana
wanaofuata njia inayo waelekeza katika maisha ya Upadre, wakimtafuta Bwana wa Kweli
wa nyakati hizi zetu. Hotuba yake kwa wanafunzi, na wafanyakaziwa Seminari hiyo,
ililenga katika Barua ya Kwanza ya Mtume Petro sura ya kwanza , mistari 3-5... Ahimidiwe
Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo! Kwa huruma yake kuu tumezaliwa upya kwa matumaini,
kupitia njia ya ufufuo wa Yesu Kristo kutoka kwa wafu, na urithi usio haribika, wala
kuwa na dosari, wala kufifia, uliotunzwa mbinguni kwa ajili yenu...... Papa Benedikto,
alitoa tafakari juu ya maandishi hayo akisema, barua hiyo ya kwanza ya Mtume Petro,
iliyoelekezwa moja kwa moja katika makanisa ya Asia , kwa namna fulani ni Waraka wa
kwanza wa Kipapa ,ulioandikwa na Askofu wa Roma wa Kwanza, unao lizungumzia kanisa
zima la Ulimwengu lkatika kila enzi. Papa Benedikto, aliendelea kueleza na kutetea
uhalisi wa uandishi wa waraka huo akisema, ina ufahamu mkubwa wa kikanisa kuhusu
mamlaka na utume wa Petro mwenyewe. Papa pia alitafakari masharti kadhaa muhimu
na mandhari ya barua, ikiwa ni pamoja na urithi, wito Mkristu katika furaha ya
kweli ya kuwa mteule wa Mungu , mahusiano ya Kikristo –katika furaha yake ya kuwa
raia wa Yerusalemu ya Mbinguni , na mamlaka za kiraia na wajibu wake , haki zake
na uwajibikaji wake katika kutunza taratibu na mielekeo na tabia yake sahihi katika
uraia wa kidunia. Na kwamba, Petro hazungumzi kama mtu binafsi lakini kama mtu
wa kanisa , katika ukuu wa uwajibikaji wake, katika usharika wa kanisa. Mtume
Petro, alifahamu hatari za kifo alizokuwa akikabiliana nazo Roma, lakini hakurudi
nyuma , aliendelea kutembea katika njia ya msalaba iliyoonyeshwa na Kristu, na hivyo
hata leo hii, anatoa mwaliko kwa watu wa leo, kuipokea imani kwa uthabiti hata kama
ni kukabiliana na kifo. Alisema, Hakuna anayeweza kuwa mfuasi wa Msulubiwa bila kukubali
pia kuyatolea katika kifo. Papa alikiambia kikundi cha vijana zaidi ya 190 ambao
wako katika majiundo yao ya kutaka kulitumikia Kanisa la ungu . Na kwa Namna ya pekee,
Papa alisema uchaguzi wao , ni uchaguzi wa namna yake , kwa maana Bwana ndiye anayemuita
kila binadamu. Daima huwa ni mapenzi ya Mungu , kwa ajili ya kuitambua sura ya Kristu
na hivyo Ukatoliki daima unakuwa ni zawadi ya Mungu. Daima tunapaswa kufurahia
hili kwa kuwa Mungu ametupatia neema hizi. Uzuri huu wa kutambua ukamilifu wa ukweli
wa Mungu na furaha ya upendo wake.