2013-02-08 15:05:14

Tanzia: Kardinali Giovanni Cheli amefariki Dunia


Tunasikitika kutangaza kifo cha Kardinali Giovanni Cheli, Rais Mstaafu wa Shirika la Kipapa kwa ajili ya Kazi za Kichungaji kwa wahamiaji na watu wasiokuwa na makazi maalum.
Kardinali Giovanni Cheli amefariki akiwa na umri wa miaka 94, na alikuwa ni Padre wa Shirika la Watakatifu Cosma na Damian. Alizaliwa tarehe 4 Octoba 1918 , Turin Italia. Alipadrishwa June 21 1942, na 8 Septemba 1978, aliteuliwa kuwa Askofu Mkuu wa Jina wa Santa Giusta, baada ya kuteuliwa Mjumbe wa Jimbo la Papa katika Ofisi za Umoja wa Mataifa. Na March Mosi, 1989, aliteuliwa kuwa Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya kazi za Kichungaji kwa wahamiaji na watu wasiokuwa na makazi ya kudumu. 21 Februari 1998, aliteuliwa kuwa Kardinali , na mwaka 2005 alipoteza haki ya kuwa mpiga kura katika Baraza la Makardinali, kwa mujibu wa umri .
Baba Mtakatifu Benedikto XV1, mara baada ya kupata taarifa za kicho cha Kardinali , kwa masikitiko amepekeleka salaam za rambirambi kwa Askofu Francesco Ravinale wa Jimbo la Asti , ambamo Papa ameonyesha kujiunga na jumuiya yote ya jimbo la Asti kuomboleza kifo hiki.
Katika salaam hizi za rambirambi, Papa amekumbuka vyema , ushirikiano wa dhati wa Marehemu katika huduma za Kanisa, alizozifanya katika ngazi mbalimbali , kwa miaka mingi, hasa katika utumishi wa Jimbo la Papa, na kanisa kwa ujumla. Papa amesema, kwa miaka yote, alishuhudia kwa shupavu wa imani kimaisha na hasa mshikamo aliokuwa nao wa kujitolea kwa ukarimu, kuutumikia wito wake wa Upadre , kama sharti msingi la muumini, na katika majiundo ya maisha ya Mkristu ya kila siku. .
Papa ametolea sala zake ili Bwana ampokeee katika ukarimu na wema wa mikono yake na amani ya milele .



















All the contents on this site are copyrighted ©.