2013-02-08 15:10:41

Mahusiano kati ya Waotodosi na Wakatoliki Urusi yatia moyo


Mahusiano kati ya Kanisa la Kiotodisi la Urusi na Kanisa Katoliki, yanaonekana kuwa katika mwendo chanya,kw amiaka ya hivi karibuni, kutokana na kutambua wazi haja ya kujenga umoja na mshikamano , kwa ajili ya kulinda maadili ya jadi ya Kikristo na kukabiliana na baadhi ya vitisho vya kisasa, kama vile fujo za ukana Mungu , ambavyo hugandamiza misingi ya maadili katika maisha ya kijamii, na kuibua migogoro dhidi ya maadili ya familia na mateso na Wakristo kubaguliwa duniani. Ni uchambuzi uliofanywa na Upatriaki kiodosi wa Urusi na kunukuliwa na shirika la habri la Asia News.
Uchambuzi huo umetazama mkazo wa majadiliano kati ya Wakristu, na hasa kati ya kanisa la Kiotodosi na Katoliki Ulaya ya Mashariki, ambako Kiongozi wa Kanisa la Kiotodosi la Moscow na Urusi yote, Patriaki Krill, hapo tarehe 2 Februari mwaka jana, akifungua Mkutano wa Baraza la Maaskofu la Kanisa la Othodoksi la Urusi, Katika hotuba yake, iliyochapishwa katika tovuti ya Upatriarki wake na kunukuliwa na AsiaNews, alikumbuka baadhi ya matukio ya kuwa pamoja katika majadiliano ya kiekumeni na Wakatoliki.
Kati ya yaliyojadiliwa katika jukwaa la kazi za kiteolojia na Maaskofu -ni muhitasari wa msimamo wa pamoja juu ya masuala kadhaa misingi, ikiwa ni mahusiano ya familia, mahusiano na serikali, kanisa, maadili na masuala ya Kiroho, na mgogoro wa kiuchumi ". Pamoja na mengine, yanayodhiririsha hatua chanya zinazopigwa katika, mwendo wa pamoja, Wakristu na hasa Waotodosi na Wakatoliki , ikiwemo ziara ya Patriaki Krill, aliyoifanya mwaka jana, Agosti, nchini Poland, ambako aliweka sahihi ya kihistoria , katika hati ya pamoja na Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Poland, Askofu Mkuu Jozef Michalik.
Hati iliyotoa iliyoonyesha dhahiri hamu ya pande zote kusamehe makosa na kuponya majeraha zamani ambayo yalikuwa yakitia uvuli katika mahusiano kati ya watu wa Urusi na Wapoland. Makanisa haya mawili kwa namna hiyo , yameweza pia kutembea katika njia ya pamoja kwa kuheshimiana, na hivyo kuwa na masimamo mmoja katika kukabiliana na mambo ya kidunia, hasa ukana Mungu, utoaji mimba, na uvujaji wa familia, na euthanasia.
Katika ujumbe wake, Patriaki Krill, ameonyesha matumaini chanya na uhusiano mzuri na Makanisa ya kale ya Mashariki, hasa ​​katika kipindi kama hiki ambapo taifa halitazamii kuona Wakristo wakichukiana wenyewe kwa wenyewe, hasa katika mtazamo wa hali ya jamii katika Mashariki ya Kati na Kusini, ambapo Wakristu ni waathirika wa mashambulizi yanayofanywa na Wababe wa Kiislamu.
Kwa Mtazamo huo, Patriaki Kirill, anatoa wito wa mshikamano kati ya Wakristo, kwa ajili ya kulinda heshima ya waumini na kulaani chuki na uharibifu dhidi ya maeneo ya kuabudu." Hatimaye, katika ujumbe wake kwa Baraza la Maaskofu, Patriaki alikosoa jumuiya za Kiprotestanti, zinazo endelea kutembea katika njia ya uhuru wa kutengana, hasa katika mafundishona maadili ya Kanisa.
Na alikosoa moja kwa moja utoaji wa baraka kwa ndoa za mashonga na madaraja matakatifu katiak Kanisa , mambo yaliyo wazi kinyume na maaadili ya kanisa, lakini yanaonekana kuwa sawa katika jumuiya kadhaa za Kiprotestanti katika Magharibi". Kwa sababu hii, alisema, ni kujaribu kuyafikia makanisa haya, ambayo yamepoteza maana yake, kupitia majadiliano na hekima, kutoa maana ya mafundisho na msimamo wa Kanisa Moja Takatifu la Kristu.








All the contents on this site are copyrighted ©.