2013-02-07 15:17:54

Padre Paolo Sottopietro kiongozi mpya wa Shirika la Udugu wa Boromeo Charles


Mkutano Mkuu wa Shirika la Udugu la Mtakatifu Boromeo Charles, Jumatano ulimchagua Padre Paolo Sottopietra, mwenye umri wa miaka 45, kuwa Mkuu mpya wa Shirika hilo. Pia Mkutano huo, uliwachagua: Vika Mkuu wa Shirika, kuwa Padre Emmanuele Silanis , na pia washauri wawili wa shirika Padre Andrea D’Ayrua na Padre Domenico Mongiello.
Mara baada ya uchaguzi huo, Mkuu mpya wa shirika akiwa ameandamana na wajumbe wa Mkutano Mkuu , wapatao 18, Mapadre wanaofanya utume wao katika bara za Afrika, Ulaya, Oceania na Amerika zote mbili walikutana na Papa siku ya Jumatano, mara baada ya Papa kutoa Katekesi yake kwa mahujaji na wageni.
Papa akikutana na wajumbe hao alionyesha furaha yake na kukiri kwmba amefarijika kwa kukutana nao. Na aliikumbuka imani thabiti na utajiri wa mawazo na ubunifu wa Padre Giussani, akisema alikulia katika urafiki wa kweli na Bwana wake. Na hivyo kupitia kwake, aliweza kuljua vyema jumuiya ya ushariki wa Mtakatifu Charles Boromeo RealAudioMP3 .








All the contents on this site are copyrighted ©.