2013-02-07 09:28:37

Kanisa na nyumba ya Parokia kujengwa nchini Cuba kama kumbu kumbu ya hija ya kichungaji ya Benedikto XVI nchini Cuba


Serikali ya Cuba imetoa ruhusa kwa Kanisa nchini humo kujenga Kanisa na nyumba ya Parokia kama sehemu ya kumbu kumbu endelevu ya hija ya kichungaji ya Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita nchini Cuba, mwezi Machi 2012. Hizi pia ni juhudi za Serikali ya Cuba kutaka kurudisha sehemu ya mali ya Kanisa iliyotaifishwa kwenye miaka ya 1960, wakati utawala wa Kikomunisti ulipokuwa umepamba moto.

Viongozi wa Kanisa wametoa shukrani zao za dhati kwa Serikali kutokana na uamuzi hii hatua ambayo itaendeleza majadiliano na ushirikiano kati ya pande hizi mbili kwa ajili ya mafao na maendeleo ya wananchi wa Cuba: kiroho na kimwili.







All the contents on this site are copyrighted ©.