2013-02-06 14:53:33

Binadamu hutambua ukuu wa Mungu pale tu ......


Binadamu huweza kuuona tu ukuu wa Mungu pale anapojitambua kwamba yeye si kitu mbele za Mungu. Baba Mtakatifu Benedikto XV1, ameeleza katika Katekesi yake ya Jumatano hii, kwa mahujaji na wageni waliokuwa wamekusanyika katika Ukumbi wa Paulo V1, Mjini Vatican.
Papa ameendelea kuifatakari sala ya Muumini akiilenga zaidi sala kuu ya Kanuni ya Imani, Nasadiki,katika mtazamo wa mwaka huu wa Imani. Alisema, Sala ya Nasadiki ambamo tunamkiri Mungu kuwa Muumbaji wa Mbingu na nchi, kama tunavyosoma mstari wa kwanza wa Maandiko Matakatifu: "Tangu mwanzo, Mungu aliumba mbingu na nchi "(Mwanzo 1:01), tunamkiri Mungu aliye asili ya mambo yote na uzuri wote wa uumbaji, unaodhihirisha uwezo wa Baba mwenye upendoā€¯.

Na hivyo , Papa alisisitiza, kupitia vilivyoumbwa nae, "Mungu hujionyesha wazi kuwa Baba wa uumbaji, katika asili ya uhai wote na katika uumbaji huo huonekana uwezo wake, kama tunavyosoma katika maandiko Matakatifu ya Biblia. Yeye, kama Baba mwema na mwenye uweza, anahudumia kila alichokiumba kwa upendo na uaminifu ambao kamwe haupungui , kama ilivyoandikwa katika kitabu cha Mzaburi.
Hivyo, uumbaji unakuwa ni mahali ambamo mna kujua na kutambua uweza wa Bwana na wema wake. Hilo kwa Muumini Mkristu unakuwa ni wito katika imani, kumtangaza Mungu kuwa ni Muumbaji. Papa alieleza na kurejea maandiko Matakatifu Mbalimbali juu ya Mungu asiye onekana kwa macho ya kibinadamu, lakini katika imani huonekana. Na hivyo imani inapata maana ya kumtambua asiyeonekana, kumtambua na kumfuatilia katika dunia ya yanayoonekana. Papa alieleza na kutoa mwaliko kwa waumini kusoma kitabu kitakatifu juu ya asili ya uumbaji na Zab 19.2-5), lakini kwa macho ya yaliyo funuliwa na Neno lake kuhusu imani, ili kuweza kuufikia ufahamu kamili wa ukweli wa Mungu kama Muumba na Baba.
Katika kazi za uumbaji, Mungu anaonekana kuwa mwenye Uweza wote, Mungu aliyeziumba Mbingu na nchi, ambaye neno lake la uzima wa milele linaleta uwepo wa ulimwengu wenye wema , maridhiano na mazuri. Na dunia hivyo, inapata maana ya kuwa ni mpango wa Mungu , mpango ambamo kwa njia ya kipekee, mwanamke na mwanamme, wanakuwa ni matokeo ya kazi ya uumbaji wa Mungu.
Maandiko Matakatifu yanatufundisha kwamba binadamu aliumbwa kwa sura na mfano wa Mungu , kutoka katika mavumbi ya aridhi . Na hapa tunaona si tu msingi wa shikamano wa familia ya binadamu , lakini pia, heshima ya utu wa binadamu usioweza kubadilishwa.
Na pia tunaliona fumbo la binadamu kama kiumbe asiyekuwa na mwisho anayeitwa kutimiza wajibu wake katika mpango wa uzima wa milele.
Kwa Adamu kutenda dhambi, aliharibu mahusiano yetu na Mungu , na kuathiri pia uhusiano na mshikamano kati ya mtu na mtu na dunia kwa ujumla. Lakini kupitia unyenyekevu wa Kristu, Adamu Mpya , Mungu mwenyewe anatufanya sisi kuwa wenye haki na kutuwezesha tena kushi kwa uhuru kama wana wake wapendwa.


Papa alihitimisha Katekesi yake kwa kuwataka Wapendwa wake kwa waume, kuishi kwa imani , na kutambua ukuu wa Mungu na kukubali udogo wetu, na udhaifu wetu kama viumbe wake na kujiruhusu kujazwa na upendo wake Bwana na kukua katika ukuu wake wa ukweli. Na kwamba , Mabaya na mashinikizo ya maumivu na mateso, tunapaswa kupokea kama fumbo lake linalomulika kutoka katika mwanga wa imani, ambao unatupa uhakika wa kuwa na uwezo wa kufunguliwa minyororo ya dhambi na uhakika wa kufurahia kuwa daima binadamu.








All the contents on this site are copyrighted ©.