Rais Barack Obama anashiriki katika mkutano wa "Kifungua kichwa cha Sala Kitaifa"
Rais wa Chama cha Uhamsho wa Roho Mtakatifu nchini Italia Bwana Salvatore Martines
kuanzia tarehe 5 hadi tarehe 7 Februari 2013 yuko Washington, DC, Marekani, kushiriki
katika majadiliano ya sala yanayomshirikisha Rais Barack Obama na viongozi wengine
waandamizi kutoka Marekani. Mkutano huu unajulikana kama kifungua kichwa cha Sala
Kitaifa au kwa lugha ya umombo wenyewe wanasema "National Prayer Breakfast".
Kuna
jumla ya wageni waalikwa 2000 kutoka pande zote za dunia na wawakilishi 160, watakaokusanyika
ili kujadili mada mbali mbali zinazoendelea kutikisa dunia katika mapambazuko ya Karne
ya Ishirini na moja. Lengo ni kuendelea na mchakato wa maboresho ya ushirikiano wa
kimataifa unaojitambulisha kwa namna ya pekee katika mshikamano, maendeleo na huduma
za kijamii zinazomgusa mtu mzima: kiroho na kimwili.
Mkutano huu kwa sasa unaingia
katika toleo la sitini na moja, umeendelea kuwa ni Jukwaa kwa ajili kujenga na kuimarisha
utamaduni wa mshimamano na udugu mintarafu tunu msingi za Kiinjili, daima wakitafuta
mafao ya wengi, haki na amani. Ni mkutano unaowashirikisha viongozi wa kidini, kisiasa
na kiuchumi,