2013-02-04 14:57:16

Yesu ni Nabii wa Ukweli na Upendo - Papa


Jumapili , akiwahutubia mahujaji na wageni waliokusanyika katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, Baba Mtakatifu Bendikto XV1, alilitafakari somo la Injili kutoka Mtakatifu Luka sura ya nne, iliyosomwa katika Ibada ya Misa ya Jumapili , akieleza kwamba katika injili hiyo, Yesu anatukumbusha sisi kwamba, kuwa Nabii si lelemama hata kwa wale walio karibu nasi.
Na hivyo, Papa alitaja umuhimu wa kuzama katika sala za kumwomba Bwana, ili kila mmoja wetu, apate ujasiri wa kiroho na hekima, kwamba maneno yetu na vitendo vyetu kama Wakristu, pia viweze kuutangaza ukweli wa upendo wa Mungu kwa uthabiti, unyenyevu na mshikamano.
Papa alieleza kwa kurejea hali halisi ya wakati wa Yesu, kwamba, licha ya kufahamika na wote katika mji wa Nazareth, alipotangaza utambulisho wake halisi katika sinagogi , kuwa ndiye Masiha , hakuna aliyemwamini. Papa alisema, pengine, ni wazi maneno ya Yesu kwa watu waliokuwa wakimsikiliza katika sinagogi kwa wakati ule, haikuwa rahisi kuuona ukweli huo, na hivyo waliona kama na kufuru. Lakini Yesu hakuhitaji ridhaa ya binadamu, kuueleza utambulisho wake asilia , kwa kuwa alikuja kuushuhudia ukweli huo.
Papa aliendelea kueleza sifa za Nabii wa kweli, kwamba hatii wala kuogopa sauti za binadamu, isipokuwa sauti ya Mungu. Ni mtu aliye tayari katika hali zote, kuhudumia ukweli, kama ilivyo thibitishwa na Yesu mwenyewe,nabii halisi wa ukweli na upendo, ulijazwa ndani mwake na Baba wa aliye juu ya yote.
Papa alieleza na kufafanua maana ya maneno haya upendo na ukweli kwamba, ni matamshi tofauti lakini yenye kuelezea uhalisi uleule.
Na kwamba kumwamini Mungu , ni kumkubali na kumfuata Yesu wa Nazareth, Nabii wa kweli . Ni kukiri kuwa ndiye Masiya, Mkombozi aliyetumwa na Mungu Baba wa Mbinguni, ili kila binadamu aaminiye na kuliishi neno lake apate kuwa na uzima wa milele.
Baada ya tafakari hii, Papa aliikumbuka tarehe 3 Feburuari , kuwa ni Siku ya Maisha, ya Kitaifa, Italia. Na hivyo kwa moyo Mkujufu alitoa shukurani zake za dhati kwa maneno yaliyotolewa na Kikundi cha Kutetea Maisha Italia cha Azione Catolica. Papa alionyesha matamanio yake kwamba, Ulaya nzima iweza kuyatetea maisha ya kila binadamu katika kila hali na kutuza heshima yake yote.








All the contents on this site are copyrighted ©.