2013-02-04 15:25:35

Tunalielekea dimbwi kubwa la hatari- Kardinali Bagnasco


Kardinali Angelo Bagnasco wa Jimbo Kuu la Genova, ambaye pia ni Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Italia, akitoa maoni yake juu ya mchakato unaoendelea kupiga hatua, katika kuruhusu sheria ya ndoa za jinsia moja huko Ufaransa, amesema unaielekeza pia Italia katika dimbwi kubwa la hatari.
Onyo hilo amelitoa baada ya Bunge la kwanza la Ufaransa kupitisha rasimu ya sheria , katika mchakato huo unaotafuta kuhalalisha ndoa za jinsia moja. Na pia amereja maoni ynayotolewa katika gazeti la Italia la kila siku la “Avvenire”yanayo shinikiza watu kukubali ndoa hizo.
Eugenio Bonanata anaripoti kwamba, Pamoja na uhamasishaji mkubwauliofanyika mitaani, watu wasikubali kuupokea muswada wa sheria ya ndoa ya mashoga, bado Bunge la Ufarasa, limepitisha rasimu ya ndoa za jinsia moja, ikiwa hatua nyingine ya kusonga mbele .
Kwa rasimu hiyo, kupiga hatua mbele , Rais wa CEI, ameionya na kuihimiza Italia isifuate Ufarasa, hasa wakati huu inapopambana na mwelekeo wa kuzama pia katika dimbwi kubwa la hatari ya utomvu wa maadili , ambao matokeo yake ni mbaya sana. Hofu ya Kardinali Bagnasco hasa inajali kwamba, kupitishwa kwa sheria hiyo, ni hatua mbele katika madai mengine ya mashoga, kupanga watoto, kama ilivyo kwa wanadoa ya mwanamke na mwanamme.
Kardinali anasema onyo lake si tu kwa nchi za Ulaya,ambazo zinasahau utamaduni wake asilia uliosmikwa katika misingi ya Kikristo, bali kwa watu wote wenye kujali maadili ya Kijamii na kumcha Mungu.
Kardinali anaamini, uhuru huu unaozidi kiasi unatafuta kuiondoa dini katika upeo wa macho ya binadamu . Na hivyo ni kufuru kubwa dhidi ya Mungu na ubinadamu."
Kardinali amesema hayo wakati wakati akiuhutumbia Mkutano wa Chama cha Vijana Katoliki cha Azione Catolica, katika kuadhimisha Siku ya Kitaifa ya Utetezi wa Maisha Italia. Ameihimiza Italia kuzingatia kwamba, familia ya mwanamke na mwanaume haianzishwi na Serikali bali sheria za serikali zinapaswa kutetea na kudumisha asili yake ya kimaadili , kiroho na kitamaduni, kama chimbuko asilia la watu.









All the contents on this site are copyrighted ©.