Zaidi ya watu 50,000 Msumbiji hawana makazi kutokana na mafuriko!
Mvua kubwa inayoendelea kunyeesha Kusini mwa Msumbiji imesababisha maafa makubwa kiasi
kwamba, hadi sasa kuna jumla ya watu 50,000 hawana makazi na kuna uwezekano mkubwa
kwamba, watu wakaendelea kupoteza maisha na mali zao.
Takwimu zinaonesha kwamba,
kuna jumla ya watu 50 wamefariki dunia kutokana na mafuriko. Wataalam wa hali ya hewa
wanasema kwamba, mafuriko ya Mwaka 2013 pengine yakawa ni makubwa zaidi kuliko yale
yaliyotokea nchini Msumbiji kunako mwaka 2000, yaliyopelekea watu zaidi ya 800 kupoteza
maisha. Waathirika wakuu ni wale wanaoishi kwenye kingo za Mto Limpopo, Kusini mwa
Jimbo la Gaza.