Moto mkubwa wateketeza bidhaa nyingi Soko kuu Bujumbura
Wafanyabiashara wengi nchini Burundi wamepoteza mali yenye thamani kubwa kutokana
na moto uliozuka kwenye soko kuu mjini Bujumbura, Jumapili, tarehe 27 Januari 2013
na kuteketeza mali iliyokuwa imehifadhiwa sokoni humo. Kutona na hasara kubwa iliyopatikana
watu wengi nchini Burundi wanahofia kwamba, bei ya bidhaa itaongezeka maradufu na
walaji walazimika kulipia hasara hii.
Inasemekana kwamba, kuna watu kadhaa
pia wanahofia kwamba, wamepoteza maisha yao, lakini habari hizi bado hazithibitishwa.
Kikosi cha zima moto kilifanikiwa kuzimisha moto huu baada ya kazi kubwa ilyowachukua
masaa kadhaa. Rais Pierre Nkurunziza aliyekuwa mjini Addis Ababa akihudhuria mkutano
wa Wakuu wa Umoja wa Afrika, alilazimika kurejea nchini mwake ili kujionea mwenyewe
hali halisi.
Baada ya kurejea nyumbani ameitisha mkutano wa dharura wa Kamati
ya Usalama ya taifa ili kuangalia hatua za kuchukua na kwamba, amewaomba Wasamaria
wema ndani nan je ya Burundi kuwasaidia watu walioathirika na moto huo.