2013-01-29 07:12:20

Maaskofu wa Kanisa la Babiloni la Caldea laanza Maadhimisho ya Sinodi kumchagua Patriaki


Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, ameitisha Sinodi ya Maaskofu wa Kanisa la Babiloni ya Caldea, itakayokuwa chini ya uongozi wa Kardinali Leonardo Sandri, Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Makanisa ya Mashariki. Pamoja na mambo mengine Sinodi hii itakuwa na dhamana ya kumchagua Patriaki wa Kanisa la Babiloni ya Caldea.

Jumatatu, tarehe 28 Januari, 2013 wameanza Sinodi hii kwa mafungo ya kiroho, wakimwomba Roho Mtakatifu ili aweze kuwasaidia katika maadhimisho ya tukio hili ambalo kimsingi linajisimika katika sala, tafakari pamoja na kumegeana uzoefu na mang'amuzi katika maisha na utume wa Kanisa.







All the contents on this site are copyrighted ©.