2013-01-26 15:43:15

Tanzia:Kardinali Joseph Glemp amefariki Dunia


Tunaskiitika kutangaza kifo cha Kardinali Josef Glemp, kilichotokea Jumatano iliyopita 23 Januari huko Warsaw Poland. Kardinal Glemp, aliyekuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Warsaw tangu 1981 hadi 2006. Amefariki akiwa na umri wa miaka 83.
Baba Mtakatifu Benedikto XV1, mara baada ya kupata taarifa ya kifo chake, alipeleka salaam za rambirambi kwa Kardinaili Kazimier Nycz wa Jimbo Kuu la Warsaw. Katika salaam hizo zilizotumwa kwa njia ya telegram, Papa amesema wema na haki, viliandamana na Kardinali Glemp, katika kazi na maisha yake yote ya kichungaji , na pia viliongoza mawazo yake katika kufikiri na kutoa maamuzi na miongozo ya utendaji wa kichungaji.
Alikuwa ni mtu wa haki katika roho ya Mtakatifu Joseph msimamizi wake na wale ambao katika mapokeo ya Bibilia walifahamu jinsi ya kuisikiliza sauti ya Mungu , na kupata utambuzi kwamba, si kwa ajili yao tu lakini pia ni kwa ajili ya jumuiya wanazozitumikia.
Utendaji wake wa haki, daima uliandamana na kutii mapenzi ya Mungu , na kusimikwa katika msingi upendo wake wa kina kwa Mungu na binadamu, ukiwa ni mwanga, uvuvio na ujasiri kwa kupambana na magumu yaliyojitokeza katika kuliongoza Kanisa wakati huo muhimu katika kufanya mabadiliko makubwa ya kijamii na kisiasa , mabadiliko yaliyofanyika nchini Poland na Ulaya kwa ujumla.
Jòsef Glemp, alizaliwa 1929 Inowroclaw Poland. Alipadrishwa akiwa na umri wa miaka 26 mwaka 1956 . Na mwaka 1979, aliteuliwa na kusimikwa kama Askofu wa Jimbo la Warmia Poland.
Baba Mtakatifu Benedikto xv1, ameendelea kuukumbuka upendo wa Kardinali kwa Mungu na Kanisa, na majitoleo ya maisha yake kwa ajili ya utetezi wa kila utu wa binadamu. Kwamba, ulimwenzesha kuwa mchungaji wa umoja dhidi ya migawanyiko , Mpatanishi mbele ya mizozo , mjenzi wa furaha iliyosimikwa katika tumaini la furaha za siku mbele, kwa tafakari za uzoefu wa mateso na huzuni ya siku za nyuma kwa Kanisa na taifa lake.
Papa ameendelea kutaja jinsi Marehemu Kardinali Glemp, alivyo endelea kufanya kazi kwa hekima na maarifa na ushirikiano wa karibu na Kardinali Stefan Wysyski wakiwa katika umoja na ushirikiano thabiti na Papa Yohane Paulo 11, kutatua masuala mengi na matatizo ya kisiasa , kijamii na maisha ya kidini kwa watu wa Poland kwa hekima kubwa. Alijiaminisha katika Kudra Takatifu ya Mungu na kutamani mema kwa ajili ya mapambazuko ya millenia mpya ambamo alianza kuiongoza jumuiya ya waamini wa Poland.
Na kipindi cha mwisho cha maisha yake alipata majaribu ya kuteswa na maradhi aliyoyapokea kwa utulivu wa kiroho. Hata katika majaribu haya alibaki kuwa shahidi imara aminifu na upendo usiokuwa na kina kwa Mungu.
Papa alimalizia salaam zake kwa kutambua moyo wa ukarimu na fadhila, uwazi na mtu asiyekuwa na mkuu . kwa Baba huyu, Kardinali Glemp, ambaye atabaki katika kumbukumbu za Kanisa si poland tu lakini duniani kote. Mungu na ampokee katika Utukufu wa ufalme wake, amina.








All the contents on this site are copyrighted ©.