Hatima ya mchakato wa Mabadiliko ya Katiba Tanzania 2013
Mchakato wa kutoa maoni kuhusu mabadiliko ya Katiba ya Tanzania unaendelea vyema kadiri
ya wachunguzi wa masuala ya kisiasa. Baraza la Maaskofu Katoliki bado linaendelea
kuwahamasisha waamini na watanzania wenye mapenzi mema kushiriki kikamilifu katika
utoaji wa maoni kwa kuzingatia mafao ya wengi, umoja wa kitaifa, haki na amani.
Leo katika sehemu
hii ya mwisho wa makala kuhusu maoni ya Katiba, Baraza la Maaskofu linaangalia kuhusu:
Kubadili Katiba, mgombea binafsi, vyama vya kisiasa, muundo wa maeneo ya uwakilishi,
ubunge na sifa zake; matokeo ya uchaguzi wa Rais, Baraza la Wazee na hatima ya Mchakato
wa maoni ya Katiba mpya. Kubadilisha Katiba Iwe wazi kutoruhusu Bunge kurekebisha
Katiba kadiri ya matakwa yao. Mabadiliko yafanyike kwa ridhaa ya wananchi. Hapa tunaweza
kubainisha na kuainisha mambo ambayo hayawezi kuguswa kabisa na Bunge. Vipengele hivyo
msingi katika Katiba vibadilishwe tu na wananchi kwa kura ya maoni. Vipengele vingine
ambavyo siyo vya msingi viruhusiwe kubadilishwa na bunge kwa kura si chini ya theluthi
mbili. (Ila hii itawezekana tu kama Katiba itawapa wananchi uwezo wa kuwawajibisha
wabunge wao kwa kuwaondosha au “recall” wasiporidhika na uwakilishi wao). Mgombea
huru/ binafsi Ni vema kuruhusu ili kuwezesha wale ambao hawapendi kujiunga na vyama
waweze kuwa na haki ya kugombea nafasi za urais, ubunge na udiwani. Hii itasaidia
pia viongozi hawa kuwajibika zaidi na kwa wananchi badala ya kujali zaidi maslahi
ya chama kama ambavyo imeonekana. Itazuia chuki na uhasama ndani ya vyama kumwondoa
mbunge ambaye ni chaguo la wananchi na wanampenda. Vyama vya siasa Ni muhimu
sheria ya kuanzisha na kuendesha vyama vya siasa ishinikize vyama vyenye kukubalika
na kuwakilisha wananchi kwa kuzingatia umoja wa Taifa na kupiga vita ubaguzi wa ukabila,
dini au makundi mangine yoyote. Vilevile kuwe na vigezo vya vyama kukubalika na wananchi
kwa kiasi cha upeo utakaokubalika. Na pia kuwe na mwongozo kuhusu matumizi na vyanzo
vya mapato ya vyama vya siasa kwa ajili ya kudhibiti rushwa na kutekwa na matajiri. Muundo
wa maeneo ya uwakilishi Maeneo haya: mikoa, wilaya na majimbo yagawanywe kwa kuzingatia
vigezo wazi: idadi ya watu, ukubwa wa eneo na hata rasilimali zilizopo. Ugawaji wa
bajeti uwe wa kuwezesha pia kuleta maendeleo kiuwiano kwa maeneo mbalimbali ya nchi
ili kusiwe na tofauti kubwa ya maendeleo baina ya kanda au maeneo mbalimbali ya nchi.
Wazo hili linakuwa wazi zaidi tunapoangalia mgawanyo baina ya Bara na Visiwani. Kumwondoa
mbunge madarakani kabla ya muda kuisha Ili kuhimiza uwajibikaji kwa wananchi, Katiba
iwape wananchi uwezo na utaratibu wa kumwondoa mbunge wao madarakani ikiwa wamethibitisha
kuwa hawafai (kwa mfano kulingana na michango yake na kura zake Bungeni kama zina
tija kwa wananchi anaowawakilisha). Elimu na ukomo wa Ubunge Kipindi cha ubunge
kiwe na ukomo wa vipindi viwili, na pia nafasi hiyo igombewe na wenye elimu isiyopungua
kidato cha sita. Kazi hiyo ina majukumu makubwa yanayohitaji upeo na uelewa na uwezo
wa kusoma na kutafiti masuala mengi. Kuhoji matokeo ya uchaguzi wa Rais, kinga
ya Rais kushtakiwa Fursa hii iwekwe ili kumsaidia mtu kujibidisha katika uadilifu
na uwajibikaji tangu aingiapo madarakani hadi anapotoka. Kuhoji matokeo inasaidia
kuondoa manung’uniko ya wale walioshindwa na kurejeshea wananchi imani kwa aliyeshinda.
Baraza la Wazee Kuwe na Baraza la Wazee lenye uwakilishi wa Kanda za kimila
(cultural zones) na Taasisi mbali mbali zinazosimamia maadili (kama za dini). Baraza
liwe pia na uwakilishi wa sehemu za jamii kama wanaume na wanawake na liwe la kushauri
na kuamua au kuafiki kuhusu mambo muhimu yanayohusu maadili, mila na uhai wa Taifa.
(Vilevile ikiwa nchi imeingia vitani liweze kuafiki kama iendelee na vita au la). NAMNA
YA KUSHIRIKI MCHAKATO Lazima kujiandaa vizuri kwa kusoma nyaraka muhimu, kuzitafakari
kwa muktadha wa maisha yetu kama Watanzania ili tuweze kutoa maoni yenye hoja nzito.
Tuongeze mwamko wetu na tujitokeze kwa wingi na kutoa maoni yetu. Mpango Tume una
hatua hizi: Kuundwa Tume Utoaji wa elimu kwa umma Kukusanya maoni : Kazi
hii imekwishaanza. Katika kila mkoa vinawekwa vituo vya mikutano hiyo. Tunaweza kutoa
maoni kwa kujieleza ama kwa kuandika. Ikiwa unashindwa kufika mkutanoni, basi andika
na kupeleka Tume au kutuma kwa njia ya posta au barua pepe. Maoni yanaweza kuwa ya
mtu mmoja ama ya kikundi. Kufanya majumuisho na uchambuzi Tume itaweka maoni
ya watu pamoja. Maoni yaliyotajwa na kuelezewa vizuri na wengi yatapewa uzito Uandikaji
wa Rasimu ya Katiba Rasimu kujadiliwa katika Mabaraza ya Katiba. Kurudisha
majumulisho kwa watu kupitia Mabaraza ya Katiba Urutubishaji / uboreshaji wa Rasimu
baada ya michango ya Mabaraza ya Katiba
Bunge la Katiba
kuijadili Rasimu Kura ya maoni Kuanza kutumika kwa Katiba mpya
Mwisho
: Ikiwa itakosa kupitishwa kwa 50% mara ya kwanza kura itarudiwa. 50% ikikosekana
tena, basi tutaendelea kutumia Katiba ya sasa hadi mchakato mwingine utakapoandaliwa.