2013-01-24 09:22:19

Siku ya Ugonjwa wa Ukoma Duniani


Tarehe 27 Januari 2013, Jumuiya ya Kimataifa itaadhimisha Siku ya 60 ya Ugonjwa wa Ukoma Duniani. Hizi ni jitihada za Umoja wa Mataifa katika mchakato wa kupambana na ugonjwa wa Ukoma, ambao licha ya juhudi kubwa zinazoendelea kutekelezwa na Shirika la Afya Duniani, lakini bado idadi ya wagonjwa wa Ukoma iko juu.

Inakadiriwa kwamba, kila siku, walau kuna watu 700 wanapata maambukizi mapya ya ugonjwa wa Ukoma. Hadi kufikia mwaka 2011 kulikuwa na wagonjwa wa Ukoma 219,075. Wagonjwa waliotibiwa ni 181, 941, kati yao, idadi ya watoto walioambukizwa Ukoma ni kubwa. Takwimu zinaonesha kwamba, kuna zaidi ya watu millioni 10 ambao wameathirika kutokana na ugonjwa wa UKOMA, hata kama wamepata tiba na kupona kabisa, bado wanaendelea kutengwa na Jamii husika.







All the contents on this site are copyrighted ©.