Waamini jifunueni katika baraka za Mungu ili mweze kuwa baraka kwa Wengine- Papa
Baba Mtakatifu Benedikto XV1, akiendelea na Katekesi juu ya sala ya Muumini, Jumatano
hii, aliielekea sala ya Nasadikiā, sala Msingi katika Imani ya Mkristu. Alisema
, katika mwaka huu wa Imani, ninapenda kutoa lafakari mfululizo juu ya sala hii, ambayo
tunaikiri. Tangu mwanzo wa Ibada, tunakiri imani yetu kwa Mungu tukisema, Nasadiki
katika Mungu, na hivyo ni uthibitisho msingi, na mwepesi katika sifa zake, na ni kujifunua
kwenye dunia isiyokuwa na ukomo, katika uhusiano na Bwana na fumbo la wokovu. Papa
aliendelea kusema, Nasadiki kwa Mungu kunamaanisha ni kushikamana Naye, kulipokea
Neno lake na kutii kwa furaha ufunuo wake. Kama inavyofundisha Katekismo ya Kanisa
Katoliki , Imani ni kitendo cha mtu binafsi , kwa uhuru wake kamili, kutoa jibu linalo
kukabiliana na mpango wa Mungu, ambaye amejifunua mwenyewe kwa Binadamu.. Kwa
maneno Mengine , tunaweza kusema, kusadiki kwa Mungu hivyo inakuwa pia ni zawadi,
kazi na Neema Takatifu na uwajibikaji wa binadamu katika utendaji wa majadiliano na
Mungu, ambaye kwa upendo , anaongea na wanadamu kama rafiki. Mungu anaongea na sisi
kwamba, katika imani na kwa imani, sisi tunaingia katika ushirika pamoja naye. Papa
alihoji ni wapi tunaweza kumsikia Mungu akizungumza na sisi? Na alitoa jibu kwamba,
Kimsingi, ni katika Maandiko Matakatifu, ambamo Neno la Mungu huweza kusikika kwa
ajili yetu na kulisha maisha yetu kama marafiki wa Mungu. Maandishi yote ya Biblia
, huzungumzia kujifunua kwa Mungu kwa binadamu. Na pia inazungumzia imani na kufundisha
imani kupitia simulizi za Kihistoria ambamo Mungu anafanikisha Mpango wake wa Wokovu
na kujiweka karibu na binadamu , kupitia watu mbalimbali, waliomsadiki Yeye na kumtumaini
Yeye, kwa utimilifu wa ufunuo wa Bwana Yesu Kristu. Papa ameeleza kwa kurejea
Maandiko Mtakatifu mbalimbali ya Biblia, historia ya ufunuo wake na kuja kwake Mwana
wake, Yesu Kristo. Tangu kufunuliwa kwa Abrahamu, baba na mfano wa waumini wote (taz.
Rum 4:11-12) anayedumishwa na baraka ya Mungu na imani katika ahadi Yake, Abrahamu
aliondoka kuelekea asipopajua. Na Vinyo hivyo kama Abrahamu, sisi pia, twaitwa
kuiachia Imani yetu, itengeneze mawazo na utendaji wetu kwa mujibu wa Neno la Kuokoa
la Mungu hata kama tunakuwa kinyume na mawazo na njia za utendaji za dunia hii. Kwa
macho ya imani, sisi tunatambua uwepo wa Mungu na ahadi yake ya uzima wa milele, zaidi
ya hali halisi ya uwepo wa usasa . Ni kujifunua wenyewe katika Baraka za Mungu , ambamo
tunaweza pia kuwa baraka kwa wengine. Baada ya Katekesi , akisalimia katia lungha
mbalimbali, Papa aliwa kumbuka wahanga wa hali mbaya ya hewa iliyokumba mji wa Jarkata
ambako mamelfu ya watu wanateswa na uharibifu wa majengo na mali uliofanywa na maporomoko
ya aridhi. Alisema katika maafa haya asilia, niko karibu na wote wanaoteswa na
hali hiyo , na aliwahakikishia ukaribu wake kupitia sala na akahimiza watu wote kuwa
na mshikamano wa karibu na wahanga hao , ili wasikose mahitaji yao muhimu.