2013-01-23 15:19:15

Miaka 30 ya Kanuni mpya sheria za Kanisa.


Baraza la Kipapa kwa ajili ya Maandishi ya Kisheria na Taasisi ya Kimataifa ya Sheria za Kanisa na Masomo linganifu ya Kidini ya Lugano Uswisss , kwa ufadhili wa Mfuko wa Joseph Ratzinger(Benedikto XV1)na Mfuko wa Yohane Paulo 11, wameandaa Mkutano wa siku moja, juu ya Kanuni na sheria za Kanisa, kama ilivyopitishwa na Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican,baada ya kufanya marekebisho katika baadhi ya kamuni na sheria za Kanisa .
Mkutano huu wa Siku moja utafanyika Ijumaa tarehe 25 Januari 2013, katika Ukumbi wa Pius X, hapa mjini Roma, kama sehemu ya kumbukumbu ya miaka 30, tangu kupitishwa kwa Kanuni hizo mpya.
Kardinali Francesco Coccopalmerio, Rais wa Baraza kwa ajili ya Maandiko ya Kisheria, Jumanne akiwasilisha tukio hili kwa wanahabari, alieleza kwamba, Mwenye Heri Yohane XXIII, katika hotuba yake ya kuitisha Mtaguso Mkuu wa Pili, mwaka 1959, alieleza haja ya Baraza kufanya mapitio katika kisheria na Kanuni za tangu 1917, ii Kanisa liweze kutembea sambamba na mabadiliko ya nyakati . "Katika mtazamo wake mpana, Papa Yohane XXIII, aliona dhahiri kwamba marekebisho ya Kanuni , yalipaswa kuongozwa na mtazamo mpya wa Kanisa unaoibuka kutoka mkutano wa kilele wa kiekumene na mkutano wa Baraza wa kimataifa.
Na Mwenye Heri Yohane Paulo II, ambaye wakati wa utawala wake, kanuni mpya zilitangazwa rasmi, pia alirudia kwamba "muundo wa baraza la Kanisa, ulihitaji marekebisho mapya, kama ilivyo sisitizwa katika Katiba ya Kanuni za Kitume 'Sacrae disciplinae leges', kwa ajili ya uhusiano wa karibu kati ya Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican na taratibu hizo mpya , akitaja kluwa ni mkamilisho wa Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican .. katika njia mbili : kwa upande mmoja, kukumbatia yaliyodhihirishwa na Baraza, na kupendekeza uwekaji na marekebisho misingi, na kwa upande mwingine , ni kuanzisha kanuni chanya kwa ajili ya utekelezaji wa Baraza ".

Kardinali Coccompalmerio, alitoa mifano mbalimbali ya dhamana ya nguvu kati ya Mtaguso Mkuu wa Pili na Kanuni za Sheria za Kanisa, akitoa mfano wa mafundisho "kuhusu Uaskofu na uhusiano kati ya Askofu na Ukuu wake katika baraza la Maaaskofu. Mfano mwingine ni Mafundisho ya Mtaguso juu ya walei na dhamira mwafaka na uhai wa waamini walei katika maisha ya Kanisa. "Mfano wa tatu ni uundaji wa parokia kama ilivyoelezwa katika Mtaguso na utekelezaji wake kisheria. Mfano mwingine ni mafundisho na marekebisho ni katika eneo la uekumeni "kama ilivyoelezwa katika nyaraka za 'Mwanga wa Mataifa, pia Kanisa Katoliki la Mashariki , na Uekumeni katika uhalisi wake.
Kardinali, alimalizia maelezo kwa kuthibitisha uwepo wa muungano wa mzuri kati ya Mtaguzo Mkuu w apili wa Vatican na Kanuni za Sheria za Kanisa kwamba , umetoa matunda ya uhuisho mpya wa maisha ya Kanisa katika maeneo mengi na ngazi nyingi.








All the contents on this site are copyrighted ©.