2013-01-21 11:11:49

Magonjwa ya mlipuko pamoja na mafuriko yanaathiri uzalishaji na tija katika sekta ya kilimo nchini Niger


Wananchi wa Niger wanaendelea kukumbana na magonjwa ya mlipuko pamoja na mafuriko mambo ambayo yanaathiri kwa kiasi kikubwa tija na uzalishaji katika sekta ya kilimo kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyeesha nchini humo. Mwaka 2012, zaidi ya watu 500,000 walilazimika kuyahama makazi yao na wengine 80 kupoteza maisha kutokana na mafuriko, bila kusahau uharibifu mkubwa uliotokea kwenye mashamba ya mpunga.

Zaidi ya watu 7,000 wamehifadhiwa kwenye Wilaya za Mkoa wa Niamey na wanahitaji msaada wa dharura, ikiwa ni pamoja na chakula, huduma ya afya na malazi. Watu wengi kwa sasa wanasumbuliwa na ugonjwa wa Malaria, kuhara na matatizo ya kupumua. Asilimia 15% ya wagonjwa wote ni watoto wadogo. Niger ni kati ya nchi ambazo zinaathirika mara kwa mara kwa mafuriko katika Ukanda wa Sahel. Licha ya mafuriko yanayoendelea, bado kuna matumaini ya kupata mavuno ya kutosha.







All the contents on this site are copyrighted ©.