Juma la Kuombea Umoja wa Wakristo siku ya Nne: kutembea kama watoto wa dunia
Katika siku hii ya nne wazo letu kuu ni kutembea kama watoto wa dunia. Kama tunatembea
katika unyenyekevu na Mungu tutahitaji kujitambua daima kuwa ni viumbe na sehemu ya
viumbe vya Mungu na hivyo wapokeaji wazawadi za Mungu. Tuepe Vitu vinavyotutenganisha
na ufahamu kwamba mahusiano na mazingira ni sehemu muhimu ya safari yetu, ya maisha
yetu na mahusiano yetu na Mungu na muumbaji, kwa kuwa yote tuliyonayo tumepewa naye
na hivyo si vyetu kuvifanyia tutakavyo. Simulizi la kikristo ni la Wokovu kwa
viumbe vyote. Ni simulizi linalojihusu - uumbaji Imani yetu ni kwamba katika Yesu,
Mungu anatwa mwili katika historia yaani katika muda na wakati unaojulikana ni imani
ambayo ni kitovu au mhimili ambamo wakristu wote wanakusanyika na kukutana. Ni
imani katika umwilisho ambayo inabeba maana na ufahamu mzima wa umuhimu wa uumbaji
wa miili, chakula, dunia, maji, na kila kinacholisha maisha yetu kama watu tunaoishi
katika sayari hii. Yesu ni sehemu kamilifu ya ulimwengu huu. Inaweza kuwa inatisha
kidogo kusikia jinsi Yesu anavyoponya kwa kutumia udongo na mavumbi, lakini ni kweli
katika maana ya ulimwengu huu ulioumbwa kama sehemu ya tendo lake la kuumba na kuleta
maisha mapya. Katikati ya ulimwengu, dunia daima hufanyiwa kazi na watu maskini,
ambao mara nyingi huwa hawashiriki katika matunda ya matokeo ya kazi, hizi ndizo onjeleo
za maskini wengi na mifano tunaijua sana katika mazingira yetu, kama kule uhindini,
kwa Wadalit. Kwa upande mwingine ni wadalit wanaotunza wanaotunza mazingira kama hekima
ya kuilima ardhi inavyoonyeshwa katika kazi. Kuitunza dunia ni pamoja na kujiuliza
swali la msingi ni kwa jinsi gani wanadamu wanaweza kuishi wakihusiana vizuri na viumbe
wengine wakiheshimu hulka yao kama watu - Dunia, utajiri na umiliki wake visiwe chanzo
cha matatizo ya kiuchumi na chemchem ya dharau kwa watu. Wakristo lazima wajiulize
hili kwa pamoja. Hatari ya kuitumia dunia vibaya na agano la kuitunza dunia linaongelewa
katika kitabu cha Walawi kuhusiana na mwaka wa Jubilee: ardhi na matunda yake havijatolewa
kwa ajili kumnyanyasa mwingine, bali ni kwa manufaa ya wanadamu wote. Hii si tunu
tu ya kidini bali inagusa pia uchumi na biashara - kwani inahusu pia ni kwa namna
gani ardhi inamilikiwa, inauzwa na kununuliwa.
SALA Mungu wa maisha tunakushukuru
kwa kutupa dunia na wale wote wanoitunza ili itupe chakula. Tunaomba Roho mtakatifu
mpaji wa uzima atusaidie kutambua kwamba sisi ni sehemu ya uumbaji wako na mahusiano
kati ya viumbe vya dunia. Tunaomba tujifunze kuitunza dunia na kusikiliza kilio cha
chake. Tunaomba tutembee pamoja na Kristu ili kuponya madonda yote tuliyosababisha
kwa dunia na kushiriki kwa haki matunda ya dunia. Mungu wa upendo tuongoze katika
njia ya haki na amani. Amina
MASWALI Masomo ya leo yanamualika Mkristo
katika kuwajibika kwa pamoja kwa kina kuhusiana na kuutunza ulimwengu. Je ni wapi
tunatekeleza kimatendo roho ya Jubilee kama wakristu kwa pamoja? Ni wapi kama
jumuia tunavikosea vitu haki hivyo kwamba tunavitumia kama nyenzo za kubeza na kuudhalilisha
ulimwengu? Ni wapi tunaweza kufanya kazi, kujifunza na kufundisha kwa pamoja juu ya
kuheshimu uumbaji na viumbe vya ulimwengu? Tafakari hii imeandaliwa na Padre Emmanuel
Nyaumba.