2013-01-17 08:22:42

Kanuni msingi katika utoaji wa maoni juu ya mchakato wa kuandika Katiba Mpya ya Tanzania


Katika utoaji wa maoni ya Katiba Mpya ya Tanzania, Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania katika mwongozo wake kuhusu mchakato huu, linawahamasisha waamini na watanzania wote kuhakikisha kwamba, wanadumisha: umoja na mshikamano wa kitaifa; maelewano na utlivu; amani na udugu. RealAudioMP3

Waamini wa Kanisa Katoliki waendelee kuchangia maoni yao wakizingatia kwa namna ya pekee: utu na heshima ya kila mtu aliyeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu; upendo, mafao ya wengi, haki msingi za binadamu, ustawi na maendeleo ya wengi nchini Tanzania.

Watanzania wanahitaji Katiba itakayojibu kero sugu na changamoto ambazo zimekuwa ni kikwazo cha maendeleo ya wengi; ijielekeze katika kudumisha haki na amani. Katiba mpya iwe ni ile Katiba inayotekelezeka na kuwajibisha. ibainishe sheria na kanuni za kupambana na saratani ya rushwa ambayo imejikita katika mihimili ya dola ambayo ni Serikali, Mahakama na Bunge.







All the contents on this site are copyrighted ©.