2013-01-06 13:43:57

Sherehe ya Tokeo la Bwana na Noeli kwa Kanisa la Mashariki ni kielelezo cha Yesu, Nuru ya Mataifa inayowaongoza watu wote!


Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana, kwenye maadhimisho ya Sherehe ya Tokeo la Bwana, Jumapili tarehe 6 Januari 2012 amekumbusha kwamba, Makanisa ya Mashariki yanaadhimisha Siku kuu ya Noeli; matukio mawili makuu yanayomwonesha Mtoto Yesu aliyezaliwa mjini Bethlehemu katika hali ya unyenyekevu, nuru ya mataifa inayowaongoza watu wote.

Katika maadhimisho ya Siku kuu ya Noeli, Kanisa linaiangalia imani ya Bikira Maria, Mtakatifu Yosefu na Wachungaji na katika Sherehe ya Tokeo la Bwana, Kanisa linayapeleka macho yake kwa imani ya Mamajusi kutoka Mashariki, waliofika mjini Bethlehemu kumwabudu Mfalme wa Wayahudi. Bikira Maria ni kielelezo cha utimilifu wa unabii ulioaguliwa kwenye Agano la Kale na Mamajusi wanawakilisha utamaduni na watu wanaomwendea Mungu, wakitafuta ufalme wa amani, haki, ukweli na uhuru.

Bikira Maria ni kielelezo cha imani ya Waisraeli iliyofunuliwa kwao kwa njia ya Manabii na inapata hitimisho lake kwa Bikira Maria aliye amini na Neno wa Mungu akafanyika mwili na kukaa kwake, kiasi cha kumwezesha Mungu kuonekana duniani. Imani ya Bikira Maria ni kielelezo cha imani ya Kanisa na Watu wa Agano Jipya na watu wote wa dunia hii, kama inavyojionesha kwa uwepo wa Mamajusi kutoka Mashariki ya mbali wanaofika Mjini Bethlehemu wakiongozwa na nyota pamoja na Maandiko Matakatifu.

Imani ya Bikira Maria inaweza kufananishwa na imani ya Abrahamu katika ahadi na mpango wa Mungu unaopata hitimisho lake katika Yesu Kristo, Mwanga angavu unawaowaangazia Mamajusi kuuona ukweli, kufika na kumwabudu Yesu Kristo; mwaliko kwa watu wote kumwabudu Mwenyezi Mungu muumbaji wa dunia, ili aweze kufahamika duniani kote.

Hiki ndicho kielelezo makini cha kuwaweka wakfu Maaskofu wakuu wapya, katika Kanisa kuu la Mtakatifu Petro, mjini Vatican, anasema Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita. Maaskofu wakuu wawili watabaki mjini Vatican kuendelea na utume wao na wawili wanatumwa kuwa Mabalozi wa Vatican. Kanisa linawaombea ili kwa njia ya utume wao, mwanga wa Kristo uweze kung'ara zaidi duniani.

Kanisa Katoliki nchini Italia, linaadhimisha Siku kuu ya Utoto Mtakatifu kama kielelezo cha mshikamano wa huruma na upendo kwa watoto wengine wanaoishi katika mazingira hatarishi: kiroho na kimwili. Baba Mtakatifu anawapongeza na kuwahimiza watoto kuwashirikisha watoto wengine upendo wa Mungu







All the contents on this site are copyrighted ©.