2013-01-05 15:01:22

Ujenzi wa Barabara Kati ya Tabora na Singida wapamba moto!


Rais Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa miradi ya barabara na daraja katika mkoa wa Tabora kuanzia tarehe 7 Januari 2013. Pamoja na shughuli nyingine, Jumatatu tarehe 7 Januari 2013 akiwa mkoani humo, Mhe. Rais kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya uzinduzi wa ujenzi wa Daraja la Mbutu liloko Wilayani Igunga.

Jumanne tarehe 8 Januari 2013, Rais ataweka jiwe la msingi la uzinduzi wa ujenzi kwa lami wa barabara
i) Nzega – Puge,
ii) Puge – Tabora,
iii) Tabora – Ndono na
iv) Tabora - Nyahua

Siku ya Jumatano ya tarehe 9 Januari 2013, Rais ataweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya Ndono hadi Urambo.

Uzinduzi wa miradi hii ni sehemu ya utekelezaji wa azma ya Serikali ya kuhakikisha kuwa makao makuu ya mikoa yote yanaunganishwa kwa barabara za lami. Miradi hii ni mafanikio makubwa katika sekta ya usafirishaji na itatoa chachu kubwa kwa uchumi wa mkoa wa Tabora na Taifa kwa ujumla. Aidha, miradi hii itasaidia sana katika kuimarisha Usafiri wa barabara kati ya Tabora na mikoa ya Kigoma, Shinyanga, Singida na Dodoma.








All the contents on this site are copyrighted ©.