2013-01-05 10:43:43

Maaskofu wakuu wateule watakaowekwa wakfu wakati wa Sherehe ya Tokeo la Bwana mjini Vatican


Ufuatao ni wasifu wa Maaskofu wakuu wateule wanaotarajiwa kuwekwa wakfu na Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, wakati wa maadhimisho ya Sherehe ya Tokeo la Bwana au Epifania, kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, hapo tarehe 6 Januari 2013.

Askofu mkuu mteule Angelo Vincenzo Zani, kutoka Jimbo Katoliki la Brescia, Italia, Katibu mkuu wa Baraza la Kipapa la Elimu Katoliki, alizaliwa tarehe 24 Machi 1950. Akapadrishwa tarehe 20 Septemba 1975 na tarehe 9 Novemba 2012 akateuliwa na Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, kuwa Katibu mkuu wa Baraza la Kipapa la Elimu Katoliki.

Askofu mkuu mteuleFortunatus Nwachukwu, kutoka Jimbo Katoliki la Aba, Nigeria, alizaliwa tarehe 10 Mei 1960. Tarehe 17 Juni 1984 akapewa daraja takatifu la Upadre. Kunako tarehe 12 Novemba 2012 akateuliwa na Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, kuwa Balozi wa Vatican nchini Nicaragua.

Askofu mkuu mteule Goerg Ganswein, kutoka Jimbo Freiburg im Breisgau, Ujerumani, alizaliwa tarehe 30 Julai 1956. Akapewa daraja takatifu la Upadre tarehe 31 Mei 1984. Baba Mtakatifu Benedikto XVI akamteua kuwa Mkuu wa Nyumba ya Kipapa hapo tarehe 7 Desemba 2012: kabla ya uteuzi huu alikuwa ni Katibu muhtasi wa Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita.

Askofu mkuu mteule Nicolas Henry Marie Denis Thevenin kutoka Jimbo kuu la Genova, Italia, alizaliwa hapo tarehe 5 Juni 1958. Akapadrishwa tarehe 4 Julai 1989. Akateuliwa na Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita kuwa Balozi wa Vatican nchini Guatemala hapo tarehe 15 Desemba 2012 na kuthibitishwa rasmi tarehe 5 Januari 2013.







All the contents on this site are copyrighted ©.