2013-01-05 12:02:06

Askofu mkuu Jean Paul Gobel ateuliwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Misri


Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, amemteua Askofu mkuu Jean Paul Gobel kuwa Balozi Mpya wa Vatican nchini Misri. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu Gobel alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Iran.

Askofu mkuu Gobel alizaliwa kunako tarehe 14 Mei 1943. Akapadrishwa tarehe 29 Juni 1969. Tarehe 7 Desemba 1993 akateuliwa na Baba Mtakatifu Yohane Paulo wa pili kuwa Askofu na kuwekwa wakfu hapo tarehe 6 Januari 1994.

Tangu wakati huo ametekeleza utume wake kama Balozi wa Vatican katika nchi zifuatazo: Armenia, Azerbaijan, Senegal, Guinea Bissau, Mali, Caper Verde, Nicaragua na Irani, utume ambao alianza kuutekeleza hapo tarehe 10 Oktoba 2007.

Wakati huo huo, Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, amemteua Askofu mkuu Nicolas Henry Marie Denis Thevenin, atakayewekwa wakfu tarehe 6 Januari 2013 kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Guatemala.







All the contents on this site are copyrighted ©.