Ujumbe kwa ajili ya Siku ya Dunia ya Amani 2013, uliotolewa na Baba Mtakatifu Benedikto
XV1, uliochapishwa hivi karibuni, umetazama kwa kina zaidi mandhari na masuala ya
kijamii, katika mahusiano na misingi ya ujenzi wa amani, miongoni mwa jamii. Na ndivyo
ilivyokuwa katika ujumbe wa Papa kwa ajili ya adhimisho la Siku kuu ya Noeli, ambamo
amelenga moja kwa moja, migogoro inayoendelea, kuanzia hali ya kutisha Syria, ambako
kuna ghasia zinazo endelea kumwaga damu ya watu bila ukomo. Na pia katika ujumbe
huo, Papa alitoa pongezi na matashi mema kwa viongozi wapya wa Jamhuri ya Watu wa
China, katika mtazamo wa majukumu yao mapya , kwenye kuihudumia taifa la China. Ujumbe
huo ulionyesha tumaini kwmaba, pengine hatua hii ya mabadiliko ya viongozi, itakuwa
ni hatua mpya katika matumaini ya kuwa na ushirikiano na kanisa katoliki , lakini
ukweli wake utajifuanua kawenye hali halisi za utendaji na utambuzi wa matarajio na
nia za Papa na Kanisa, kutembea pamoja katika njia ya ubinadamu. Pia ni juu ya Idadi
kubwa ya watu wa China ambao ni sawa na moja ya tano ya watu wote duniani,kujiunga
katiak mizania hii ya dunia ya ubinadamu. Na pia kwa ajili ya uhuru wa kidini
kwa watu hao kama hitaji muhimu katika ujenzi wa jamii yenye mshikamano na ushirikiano
kama Mapapa walivyohimiza kwa mfululizo bila kuchoka, kwamba dini haipaswi kuchukuliwa
kama uvujaji wa sheria au uhalifu, au kama sababu ya kuwatenganisha watu au kuingiliwa
nje, lakini kama vikosi chanya vya kiroho , vilivyo tayari kuchangia kwa manufaa
ya wote. Kwa roho hii ya umoja na ushirikiano, Jimbo la Papa, daima huijali
jamii Katoliki nchini China, kama ambavyo daima limekuwa wazi na nia hii katika ujumbe
wote uanopelekwa China na Mapapa wote. Katika tahariri hii , Padre Federico Lombardi
anahoji, iwapo kutakuwa na matumaini hayo katika Mwaka mpya . Na ameyaweka matumaini
hayo kwa Mfalme wa Amani, aliye kuja duniani kwa ajili ya watu wote, wanaoishi katika
mataifa madogo na makubwa. "Kama twaitafuta amani , wadogo hawapaswi kuwa na hofu
dhidi ya wakubwa. La sivyo, ni wazi kutakuwa na woga". Na kwamba Papa alitoa
Salaam hizi za matashi mema ya amani katika lugha 65,ambazo zilitakiwa kutamkwa katika
maelfu ya lugha zote ulimwengu, kwa sababu sisi sote ni familia moja ya binadamu
na tuna Baba mmoja.